22.6 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 17, 2024

Contact us: [email protected]

JPM awaagiza waajiri kuzingatia sheria ya afya, usalama kazini

Mwandishi Wetu, Mbeya

RAIS Dk. John Magufuli, amewataka waajiri na wamiliki wa sehemu za kazi wote kuzingatia utekelezaji wa Sheria ya Afya na Usalama Mahali pa Kazi ya mwaka 2003 pamoja na sheria nyingine za kazi ili kuboresha mazingira ya kazi hapa nchini.

Kauli hiyo aliitoa wiki hii alipowahutubia wafanyakazi na wananchi waliokusanyika katika Uwanja wa Sokoine kusherehekea siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi).

“Lakini kuhusu uboreshaji wa mazingira na usalama sehemu za kazi natoa wito kwa waajiri wote kuhakikisha wanazingatia sheria za kazi ikiwemo Sheria ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi. Aidha, waajiri hawana budi kutekeleza matakwa mengine ya kisheria ikiwamo kutoa mikataba ya ajira na kuruhusu uwepo wa vyama vya wafanyakazi katika sehemu za kazi,” alisema Magufuli.

Kauli yake hiyo ilikuwa inajibu hoja mbalimbali zilizotolewa na hotuba ya Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (Tucta), katika hotuba yao iliyowasilishwa katika sherehe hizo na Katibu Mkuu wake, Dk. Yahya Msigwa, aliyesema uwapo wa baadhi ya waajiri ambao hawazingatii masharti ya afya na usalama mahali pa kazi kama Sheria ya Osha inavyoelekeza.

Pia suala hilo la uzingatiaji wa Sheria ya Afya na Usalama Mahali pa Kazi lilielezwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, aliyoiwasilisha katika sherehe hizo na alifafanua juu ya tozo mbalimbali za Osha zilizoondolewa ili kuboresha mazingira ya biashara miongoni mwa wawekezaji.

“Nafurahi kukwambia sisi katika ofisi ya Waziri Mkuu tuliwaagiza Osha wahakikishe wanaondoa tozo zote ambazo ni kero. Kwa mwaka wa fedha unaoishia mwaka huu, tayari Osha wameshaondoa tozo zifuatazo; tozo ya usajili iliyokuwa inaanzia shilingi 50,000 hadi 1,800,000, ada ya fomu ya usajili sehemu za kazi, wamefuta pia faini zilizokuwa zinahusiana na vifaa vya kuzimia moto shilingi 500,000, tumeondoa ada ya leseni kwa matakwa ya sheria na tumewaambia Osha watafanya kazi hiyo kwa kuwa Serikali imewaajiri hawana tena nafasi ya kuendelea kukusanya tozo ya leseni, lakini watawajibika kuendelea kutoa leseni kwa waajiri wanaofuata masharti ya kulinda afya na usalama mahali pa kazi,” alisema Mhagama.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles