20.8 C
Dar es Salaam
Saturday, August 20, 2022

JPM atoa zawadi ya viwanja kwa wachezaji, bondia na viongozi wao

Anna Potinus-Dar Es Salaam

Kufuatia ushindi wa Taifa Satrs wa 2-1 dhidi ya timu ya taifa ya Uganda uliotuwezesha kupata tiketi ya kufuzu mashindano ya Mataifa ya Afrika yatakayopigwa Misri, Rais Dk John Magufuli ametoa zawadi ya viwanja vya kujengea nyumba Mkoani Dodoma kwa wachezaji, viongozi wao na bondia Hassan Mwakinyo kama ishara ya kuonyesha alivyofurahishwa kwa juhudi za pamoja kwa wachezaji na viongozi wao.

“Nimeamua niwape zawadi kidogo kwa niaba ya watanzania, nitawapatia viwanja vya kujenga nyumba wachezaji wote wa Taifa Stars na viongozi wao, bondia Hassan Mwakinyo pamoja na mwalimu wako, zawadi hiyo pia kwa Peter Tino na Leodegar Tenga,”

Rais Magufuli katika kutekeleza hilo amemuagiza Waziri Mkuu asimamie upatikanaji wa maeneo mazuri mkoani humo ili kila mmoja apate kiwanja chake na ikiwezekana lipatikane eneo moja ili watakapostaafu maisha yao yasiwe ya ajabu.

Rais Magufuli ametoa zawadi hiyo leo Machi 25 alipokutana na wachezaji wa Taifa stars, Viongozi wa TFF, Kamati ya uhamasishaji na bondia, Hassan Mwakinyo Ikulu jijini Dar Es Salaam, katika hafla ya kuwapongeza na kula nao chakula cha mchana.

Katika mazungumzo hayo yaliyohudhuriwa na Makamu wa Rais, Samia Suluhu na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa rais Magufuli amewapongeza wachezaji hao kwa mchezo mzuri waliocheza na amewataka waongeze bidii lakini amesisitiza akiwataka waache kujiona kwamba ndio wachezaji bora kwa kushinda huko.

“Inawezekana mlivyoshinda jana viburi vimewajaa, mnaweza mkatoka hapa mkijiona ni wachezaji wazuri halafu makaenda kwenye mashindao turudi tena kama tulivyokuwa zamani, ninawaomba vita sasa ndio imeanza,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
199,058FollowersFollow
551,000SubscribersSubscribe

Latest Articles