27.6 C
Dar es Salaam
Sunday, November 28, 2021

Jamii kutumia fursa za vikoba kujikwamua

Na UPENDO MOSHA-MOSHI

JAMII imetakiwa kuzitumia fursa zitokanazo na Vicoba kwa ajili ya kuanzisha miradi mbalimbali ya kiuchumi katika maeneo yao ili waweze kujiajiri wenyewe hatua ambayo itasaidia kujikwamua na hali ngumu ya maisha.

Hayo yalibainishwa na Mratibu wa Mradi wa Vicoba Shirikishi kupitia shirika la TUSONGE,  Helen Mushi, wakati akizungumzia mradi wa Vicoba , kwa watu wenye ulemavu na wasio na ulemavu unaotekelezwa katika kata ya Njia Panda Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro.

Alisema Vicoba imekuwa mkombozi mkubwa kwa wananchi wengi na endapo wakivitumia vyema watajikwamua kwenye umasikini na kuweza kusaidia harakati za Serikali kuifanya Tanzania kuwa ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Mushi alisema kuanzishwa kwa mradi huo kumeweza kuwaunganisha watu wenye ulemavu na watoa huduma kwa  watu wenye ulemavu na kwamba kupitia mradi huo wameweza kunufaika.

“Uwepo wa Vicoba kumesaidia kwa kiasi kikubwa cha wananchi hususani wale wa kipato cha chini na cha kati kujiinua kiuchumi ikiwemo walemavu hivyo ni vema wakatumia fursa ya vicoba kujiondoa katika umasikini.

“Watu wenye ulemavu wanashindwa kufikia taasisi za kifedha husani benki kutokana na umbali, lakini pia taratibu za kibenki hazikopeshi jamii kwa urahisi, hivyo kuanzishwa kwa vicoba hivi kutasaidia watu wa hali ya chini kuweza kukopeshana na kuinuana kiuchumi. 

“Kwa awamu ya kwanza ya utekelezaji wa mradi huu,  TUSONGE tumeweza kuwafikia wanufaika 85, ambapo wanufaika wa mradi wako 180 na kwa mwaka 2018/2020, watu wenye ulemavu wa moja kwa moja 30, wazazi wenye  ulemavu nyumbani 55 ,”alifafanua Mushi.

Aidha aliongeza kusema kuwa mradi huo umefadhiliwa na mashirika mawili ya Serikali ya Uingereza, ambayo ni African Initiatives na Big Lottery Fund, lengo ni kuwaunganisha watu wenye ulemavu ili na wao wajione kama sehemu ya jamii.

“Shirika la Tusonge tumeona kwamba kuna uhitaji mkubwa wa kuanzisha vikundi kwa watu hawa wenye ulemavu ikiwa pia ni elimu ya kujitambua, mradi mzima umewagusa wanufaika 85  ambao kwa kupitia Vicoba wameweza kujiwekea akiba na kukopeshana,” alifafanua Mushi.  

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,186FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles