26.8 C
Dar es Salaam
Saturday, September 7, 2024

Contact us: [email protected]

Iran yaapa kujilinda kwa nguvu zote kwa watakaoichokoza

BAGHDAD, Irak

WAZIRI wa Mambo ya Kigeni nchini Iran , Mohammad Javad Zarif, amesema nchi yake itajilinda kwa nguvu zote dhidi ya uchokozi wa kijeshi na kiuchumi, huku akizitolea wito nchi za Ulaya kuchukua hatua zaidi kuyanusuru makubaliano ya nyuklia waliyotia saini.

Akizungumza jana kwenye mkutano na waandishi habari mjini hapa,  Zarif alisema kwamba nchi yake inataka kujenga uhusiano wa usawa na jirani zake katika  eneo la Ghuba na imekwishapendekeza kutiwa saini mkataba wa kuepuka uchokozi.

Wakati huo huo, Rais Hassan Rouhani wa Iran ameashiria kuwa Iran inaweza kuitisha kura ya maoni kuhusu mpango wa nyuklia wa nchi hiyo kufuatia kuongezeka mvutano kati yake na Marekani.

Rouhani amesema amewahi kupendekeza suala hilo kwa Kiongozi wa Mkuu Ayotallah Ali Khamenei mwaka 2004 alipokua mjumbe mwandamizi kwenye mazungumzo ya nyuklia.

Kura hiyo ya maoni itaipa serikali ya Iran uhalali wa kisiasa iwapo itaamua kuongeza urutubishaji wa madini ya urani unaozuiwa chini ya makubaliano ya 2015 na mataifa yenye nguvu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles