26.8 C
Dar es Salaam
Saturday, September 7, 2024

Contact us: [email protected]

Facebook yadhibiti akaunti za uchaguzi Afrika

SAN FRANCISCO, MAREKANI

KAMPUNI ya Facebook inayomiliki mtandao huo wa kijamii, imetangaza kufuta mamia ya akaunti za watu kwenye mtandao huo na kupiga marufuku kampuni ya Israel kutokana na inachotaja kuwa tabia za uongozi zilizoratibiwa na zinazolilenga Bara la Afrika.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mmiliki wa kampuni hiyo, Mark Zuckerberg, akaunti nyingi zimebainika kuwa bandia na mara nyingi huweka taarifa za kisiasa, ikiwemo chaguzi katika baadhi ya mataifa.

Facebook imekabiliwa na shutuma kwa kushindwa kudhibiti taarifa za uongo katika jukwaa hilo la mtandao wa kijamii. Mwaka 2016, mtandao huo ulizindua programu ya kuangalia uhakika wa taarifa muda mfupi baada ya Rais Donald Trump wa Marekani kuingia madarakani.

Katika ujumbe kwenye blogu, Facebook imesema imefuta akaunti 265 kwenye mtandao huo zilizofunguliwa nchini Israel na zilizoilenga Nigeria, Senegal, Togo, Angola, Niger na Tunisia pamoja na kushuhudiwa sehemu ya shughuli zake Amerika Kusini na Kusini Mashariki mwa Asia.

Imesema kuwa walikuwa na majina kama ‘Hidden Africa’ na siri ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo. Ujumbe huo ulionekana kumuunga mkono rais mpya, Felix Tshisekedi na kumwomba mgombea wa upinzani akubali kushindwa.

Kwa upande wake Nathaniel Gleicher, mkuu wa kitengo cha kupambana na uhalifu wa mtandaoni katika Facebook, amesema: “Watu wanaohusika na mtandao huu walitumia akaunti bandia kuendesha kurasa hizo, kusambaza taarifa zao na kuongeza mawasiliano kwa njia za uongo.

Walijifanya kuwa watu kutoka mataifa hayo, wakiwemo kutoka vyombo vya habari nchini na kuchapisha na kutuhumiwa kufichua taarifa kuhusu wanasiasa.”

Ameongeza kwa kusema uchunguzi umebaini kwamba shughuli hizo zimehusishwa na kampuni ya Israeli ya Archimedes Group.

“Shirika hilo na matawi yake sasa yamepigwa marufuku kutoka Facebook na kupewa onyo kali la kusitisha shughuli hizo,” amesema Nathaniel Gleicher.

Wahusika wa akaunti hizo walitumia dola 812,000 kwa matangazo kati ya Desemba 2012 na Aprili 2019, Facebook imesema na fedha hizo zimelipwa kwa kutumia sarafu ya Real (Brazil), Shekel (Israel) na Dola za Marekani.

Nchi tano kati ya 6 za Afrika zilizolengwa zimekuwa na uchaguzi tangu 2016 na Tunisia itaandaa uchaguzi baadaye mwaka huu. Facebook imeshutumiwa kwa kushindwa kukabiliana na habari ghushi ambazo zinaweza kuathiri namna watu wanavyopiga kura katika uchaguzi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles