30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Mwanjelwa atoa onyo kwa ofisa utumishi Kibaha

DMWANDISHI WETU-PWANI

NAIBU Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dk. Mary Mwanjelwa, amempa onyo kali Ofisa Utumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha,  Ruth Mwelo ambaye ni Mkuu wa Idara ya Utawala na Rasilimaliwatu wa halmashauri hiyo kwa kumtolea lugha chafu mstaafu aliyekuwa akidai haki yake na kumtaka afisa huyo ajirekebishe haraka iwezekanavyo.

Onyo hilo amelitoa juzi wilayani Kibaha, wakati wa kikao kazi na watumishi wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha na Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji, kabla ya kutembelea wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika wilaya hizo ili kujiridhisha na utekelezaji wake.

Alisema haiwezekani afisa huyo mwenye dhamana ya kusimamia Sheria, Kanuni na Taratibu za kiutumishi ndio awe kikwazo cha utendaji kazi katika halmashauri hiyo kwa kutoa lugha chafu dhidi ya wanaofuta huduma ofisini kwake.

“Ofisa huyu ndiye anayestahili kuwa kwenye Kamati ya Maadili ili kutoa miongozo ya uadilifu na kusimamia maadili ya watumishi kwa ujumla katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha sasa inakuaje anafanya hivi?,” alisema na kuhoji

Kutokana na hali hiyo alimtaka ofisa huyo kutotumia cheo chake vibaya na badala yake asimamie vema nidhamu na masilahi ya watumishi wa umma.

Licha ya hali hiyo pia amemtaka kuacha tabia ya kutoa siri za ofisi na kutokuwa mchonganishi miongoni mwa watumishi wenzie kwani matendo hayo hayapaswi kufanywa na mtumishi yeyote nchini.

Dk. Mwanjelwa alisema ameliweka bayana suala la upungufu wa ofisa huyo mbele ya watumishi wenzie ili ajifunze kutokana na matendo yake yasiyoridhisha na aweze kubadili mwenendo wake mbaya wa kimaadili.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles