23.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Mwakyembe awalipua viongozi TFF

MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe, amewashangaa viongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kushindwa kuhudhuria na kuvumbua vipaji katika michuano ya Majeshi iliyofikia tamati juzi, Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Dk. Mwakyembe aliyasema hayo katika hafla ya kuwapongeza wachezaji wa timu zote za majeshi ya ulinzi kutokana na kuonyesha vipaji vya michezo mbalimbali katika michuano hiyo.

Alisema ni aibu kwa viongozi wa TFF ambao ni baba wa soka hapa nchini, kushindwa kujitokeza katika michuano hiyo ambayo alidai kwa upande wa soka vilionekana vipaji vingi.


“Nashangaa kuona hakuna mtu wa TFF hata mmoja hapa, nimesikitika sana kuona watu wangu hawakuwepo pale na hawana hata habari.

“Mchezo huu wa fainali vijana wameonekana wana utimamu wa hali ya juu, dakika 90 utafikiri ndio kaanza kucheza, lakini TFF wako bize na wachezaji sijui kutoka wapi wanaowaita Taifa Stars,” alisema Mwakyembe kwa masikitiko.

 Alisema baada ya kufika uwanjani hapo alitegemea kuwaona viongozi wa TFF wakifanya skauti ili kusaka vijana wazuri watakaounda timu ya Taifa siku sijazo, lakini alishangaa kutowaona hatua iliyomfanya aamini bado kuna safari ndefu ya kusaka mafanikio katika michezo.

 “Jeshi letu ni chombo adimu tunajivunia mmetupa heshima kubwa sana duniani kulinda heshima ya nchi yetu, nawapongeza viongozi wa ulinzi na usalama kwa kazi kubwa, hasa upande wa michezo,” alisema.

 Alisema mwaka jana alihudhuria mbio za Kilimanjaro Marathon na kubaini uwapo wa washiriki wengi kutoka Kenya ambao walizoa zawadi ya mshindi wa kwanza mpaka 30, hatua ambayo haikumfurahisha na kutamani Mlima Kilimanjaro ufunuke umfukie.

“Baada ya mbio niliwashauri wakae na jeshi kwa kupanga ratiba yao vizuri, ili kupata wachezaji.

“Niliwaambia jeshini kuna wachezaji wengi na wazuri, ila safari hii vijana wawili wa kutoka jeshi ndio wametutoa aibu katika mbio za kilomita 42 na 21.

 “Jeshini kuna vipaji vingi sana na uwezo mkubwa wanao, hata mchezo wa fainali kati ya SMZ na Ngome ulikuwa wa kukata na shoka,” alisema.

 Kwa upande wake Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Venance Mabeyo, alimshukuru Mwakyembe kwa kukubali mwaliko wao na kujumuika nao.

Alisema wamefarijika baada ya kuona

 waziri mwenye dhamana ya michezo amejumuika nao.

“Nawapongeza wanamichezo wote kwa kucheza michezo na kumaliza mashindano salama, matokeo mazuri mliyoyapata ni kutokana na maandalizi mazuri mliyoyafanya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles