31.2 C
Dar es Salaam
Saturday, August 13, 2022

Brazil yamkamata rais wa zamani

RIO DE JANEIRO, BRAZIL

ALIYEWAHI kuwa Rais wa Brazil, Michel Miguel Elias Temer Lulia, amekamatwa katika operesheni ya uchunguzi wa makosa ya ulaji rushwa inayoendelea nchini humo na kujulikana kwa jina la Operation Car Wash.

Kwa mujibu wa mtandao wa gazeti la Rio Times, umeripoti kuwa Rais Temer ambaye alikuwa wa 37 nchini Brazil na mwenye umri wa miaka 78 ambaye aliongoza nchi hiyo kuanzia Agosti 31, 2016 hadi Desemba 31, 2018 anatuhumiwa kwa makosa mbalimbali ya ufisadi.

Mwanasiasa huyo anatuhumiwa kuwa kiongozi wa kundi la uhalifu linalojihusisha na utakatishaji fedha na ubadhirifu nchini humo. Rais huyo wa zamani pia anatuhumiwa kupokea hongo, ikiwa ni pamoja na inayohusishwa na ujenzi wa kiwanda cha nyuklia cha Angra dos Reis katika Jimbo la Kusini mwa Jiji la Rio de Janeiro.

Temer ni rais wa zamani wa tatu mfululizo nchini Brazil kukabiliwa na mashtaka ya uhalifu, baada ya Luiz Inacio Lula da Silva na mwanafunzi wake, Dilma Rousseff.

Uchunguzi huo wa ufisadi ulioanza Mei mwaka 2014, umewanasa wanasiasa wengi nchini Brazil pamoja na makampuni kadhaa makubwa, kama vile kampuni kubwa ya ujenzi ya Odebrecht na hasa kampuni ya mafuta ya Brazil inayomilikiwa kwa sehemu na Serikali ya Petrobas.

Michel Temer alichukua madaraka Agosti 2016, baada ya mtangulizi wake, Dilma Rousseff, kuvuliwa madaraka na Bunge kwa tuhuma za rushwa na matumizi mabaya ya nafasi yake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,625FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles