25.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 29, 2021

BoT yataja faida za dhamana za serikali

Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM

WATANZANIA wameshauriwa kushiriki kikamilifu katika minada ya dhamana za Serikali kwani faida zake ni kubwa kwa Taifa ikiwamo kufanya shughuli za maendeleo kwa kutumia fedha zake za ndani.

Hayo yamesemwa hivi karibuni mjini Dodoma na Mkurugenzi wa Masoko na Fedha wa Benki Kuu ya Tanzania(BoT),  Alexander Ng’winamila wakati akiwasilisha mada katika mafunzo kwa waandishi wa habari za uchumi na fedha yalioandaliwa na BoT kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kuandika habari za fedha na uchumi.

Akizungumza wakati akitoa mada inayohusu uwekezaji katika dhamana za Serikali; faida zake kwa Taifa na wawekezaji ambapo pamoja na mambo mengine amezungumzia umuhimu wa wananchi kushiriki kikamilifu kwenye midana ya dhamana za Serikali.

Alisema bado kuna haja kwa vyombo vya habari kuendelea kutoa elimu kwa wananchi ili waweze kujua na kushiriki kikamilifu  katika minada hiyo.

“Ombi letu kwa vyombo vya habari tunaomba muendelee kuelimisha umma kuhusu umuhimu wa kushiriki kwenye dhamana za Serikali. Kuna faida nyingi na mojawapo ushiriki wao utawezesha Serikali kutekeleza miradi ya maendeleo kwa kutumia fedha za ndani badala ya kwenda kukopa nje ya nchi,” alisema Ng’winamila

Alifafanua faida zinazopatikana kwenye dhamana za Serikali ikiwamo kusaidia serikali kugharamia bajeti iwapo kutakuwa na upungufu wa kibajeti, kupata fedha za kuendeshea miradi ya maendeleo, kusimamia ujazi wa fedha katika uchumi pamoja na kudhibiti mfumuko wa bei.

Alisema hutoa fursa za uwekezaji ,hivyo kuwepo kwa ushindani katika uwekezaji mbalimbali na kusaidia kupatikana kwa riba zinazoaminia na soko huku akieleza kwa mwananchi wa kawaida faida

Alitaja faida nyingine dhamana za Serikali zinahamishika hivyo mwekezaji anaweza kuuza muda wowote pamoja na dhamana hizo zinaweza kutolewa kama dhamana kwa ajili ya mikopo.

Akizungumzia kuhusu minada ya dhamana za Serikali alisema ipo ya aina mbili ambapo kuna mnada wa muda mfupi ambao ni wa mwaka mmoja na mnada wa dhamana za Serikali wa muda mrefu ambao unaanzia miaka miwili mpaka miaka 20.

Alisema fomu za kujiunga zinapatikana kupitia mawakala waliopo nchini pamoja na kwenye tovuti ya Benki Kuu ya Tanzania ambapo ametumia nafasi hiyo kufafanua unapozungumzia dhamana za Serikali kwa lugha rahisi ni kwamba Serikali inakopa kwa wananchi wake.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,277FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles