23.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 8, 2021

Bodi ya Mikopo kuanza msako kwa wadaiwa

CHRISTINA GAULUHANGA-DAR ES SALAAM

BODI ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HSLB) imesema  itaanza msako mkali wiki hii kuwasaka wanufaika zaidi ya 109,980 ambao hawajanza kurejesha Sh bilioni 291.5.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdul- Razaq Badru alisema fedha hizo zinatakiwa ziwe tayari zimekusanywa  wahitaji wengine waendelee kunufaika na mkopo huo.

“Hadi Juni mwaka huu tunatakiwa wadaiwa sugu hawa wawe tayari wamerejesha fedha hizi wengine nao waweze kunufaika nazo,” alisema Badru.

Alisema pia wiki ijayo itaanza kazi ya kuwatembelea waajiri kwa lengo la kuwatafuta wanufaika ambao hawajaanza kurejesha au wale ambao wamerejesha  kiwango kisichofuata matakwa ya serikali.

Badru alisema katika kipindi cha mwaka huu wa fedha wamepanga kukusanya Sh bilioni 150 wakati malengo ya makusanyo katika   miezi sita (Julai hadi Desemba) yalikuwa ni Sh bilioni 71.4.

 “Katika kipindi cha Julai hadi Desemba mwaka 2018 tumeweza kukusanya Sh bilioni 94.01  sawa na ongezeko la asilimia 8.7 ikilinganishwa na Sh.bilioni 85.88 zilizokusanywa kipindi kama hicho  mwaka uliopita (Julai hadi Desemba 2017),”alisema Badru.

Alisema makusanyo hayo yalikuwa ni ya wanufaika 198, 659 ambao wameajiriwa au kuajiriwa katika sekta binafsi na umma.

Akizungumzia hali ya ukusanyaji katika kipindi cha miaka minne alisema walikusanya Sh bilioni 21.7 mwaka (2014/15), Sh bilioni 28.2 (2015/16), Sh bilioni 116.7 (2016/17), Sh bilioni 181.4 (2017/18 na Sh bilioni 94.01 (2018/19, (ambazo ni za Julai hadi Desemba 2018).

Alisema tayari wamejiunga na mfumo wa Serikali wa Ukusanyaji Mapato wa (GePG),  hivyo kuwataka wanufaika na waajiri kuanzia sasa kutumia mfumo huo unaotumiwa na taasisi mbalimbali za serikali.

Alitoa wito kwa waajiri kutekeleza masharti ya Sheria ya HESLB inayowataka kukata asilimia 15 ya mshahara ghafi na kuwasilisha makato ndani ya siku 15 baada ya mwisho wa mwezi.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,549FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles