24.2 C
Dar es Salaam
Monday, August 8, 2022

Aussems apania kuipa Simba ubingwa wa Afrika

MWAMVITA MTANDA-DAR ES SALAAM

BAADA ya Simba kupata ushindi wa mabao 2-1 katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi wa Ligi ya Mabingwa Afrika ambao umewapa nafasi ya kutinga hatua ya robo fainali, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Patrick Aussems, amesema atapambana kuhakikisha kikosi chake kinachukua ubingwa wa Afrika.

Simba ilitinga hatua hiyo baada kupata ushindi katika mchezo huo uliochezwa juzi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Ushindi huo uliifanya Simba kufikisha pointi tisa na kumaliza kwenye nafasi ya pili kwenye msimamo wa kundi hilo nyuma ya Al alhly ya Misri iliyomaliza na pointi 10, JS Soaura iliyomaliza nafasi ya tatu ikiwa na pointi nane, wakati AS Vita ikimaliza mkiani na pointi zake saba.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Aussems alisema mipango yake kwa sasa ni kuhakikisha wanafanikiwa kuchukua ubingwa wa michuano hiyo.

Alisema awali walikuwa na malengo ya kufikia hatua ya makundi ya michuano hiyo, lakini baada ya kufanikiwa alipata morali iliyopelekea asonge mbele zaidi.

“Nitapambana kwa hali na mali kuhakikisha kuwa Simba inafanikiwa kuchukua ubingwa, hakuna sababu  ya kuhofia timu yoyote ambayo tutakutana nayo, nina imani timu yangu inaweza na ndio maana mpaka hapa tumefanikiwa kwa kiasi kubwa sana,” alisema Aussems.

 “Nataka Simba iweke historia mwaka huu ipate ubingwa wa Afrika na pia ishinde tena michuano ya Ligi Kuu, hata kama nitaondoka basi nitakuwa nimeacha historia nzuri,” alisema Aussems.

 Aussems alimmwagia sifa kiungo wake, Haruna Niyonzima, kwa kiwango alichokionesha katika mchezo huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,235FollowersFollow
549,000SubscribersSubscribe

Latest Articles