30.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Zungu kusaka viwanda bubu vya vifungashio

Christina Gauluhanga – Dar es Salaam

WAZIRI Nchi Ofisi wa Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mussa Zungu amesema kuwa ofisi yake itaendelea kuwasaka wenye viwanda bubu wanaozalisha kinyemela vifungashio visivyo na kiwango ambavyo vina athari kiafya.

Alieleza mkakati wa Serikali kupiga marufuku uzalishaji wa vifungashio visivyo na viwango, lakini bado kuna viwanda bubu mitaani vinavyoendelea kuzalisha na baadhi ya nchi zinaleta hapa nchini.

Akizungumza jana Dar es Salaam, Zungu alisema mbali ya kuharibu mazingira, lakini vifungashio hivyo vina athari za kiafya kwa sababu baadhi ya malighafi wanazotumia zimetokana na ubebaji wa saruji na mbolea kali ambazo zina athari kiafya.

“Serikali imejipanga vema kutunza mazingira na kuzuia vifungashio visivyo na ubora, lakini bado kuna baadhi ya wananchi wanapenyeza bidhaa hizo ambazo hazina viwango na hazijapitishwa na mamlaka zinazohusika, tutawasaka na kuwachukulia hatua,” alisema Zungu.

Alisema vifungashio hivyo si imara hata kwa kubebea bidhaa, hivyo amewataka wananchi kutumia vifungashio vyenye muhuri na vilivyopitishwa na mamlaka husika kwa matumizi.

Wakati huohuo, Zungu aliahidi kuendeleza kushirikiana na Manispaa ya Ilala kwa kuwa ndio imemng’arisha hadi Serikali imemuona.

“Ninaomba Allah (Mwenyezi Mungu) aniongoze, siwezi kutengana nanyi au kukosa kikao hata kimoja cha baraza hili kwa kuwa nafahamu umuhimu wake,” alisema Zungu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles