24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Zitto aelezea simu yake ilivyodukuliwa, ataka msaidizi wake aliyetekwa aachiwe

Anna Potinus, Dar es Salaam

Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, ameelezea simu yake ilivyodukuliwa akihusisha tukio hilo na lile la kutekwa kwa msaidizi wake, Raphel Ongangi raia wa Kenya.

Kutokana na hali hiyo, Zitto amewataka watekaji hao kumwachia huru kwani hana taarifa zake wanazozihitaji.

Raia huyo wa Kenya anadaiwa kutekwa na watu wasiojulikana jijini Dar es Salaam, wakati akitoka shuleni kwa watoto wake kwenye kikao cha wazazi.

“Siku mbili baada ya Raphael kutekwa, akaunti zangu za mitandao ya kijamii zilidukuliwa na Raphael alikuwa na password zangu, hata hivyo hana taarifa zozote juu yangu hivyo ninawaambia watekaji hawawezi kupata taarifa zozote juu yangu kutoka kwa Raphael kwasababu watamtesa bure na hana taatifa ambazo anaweza kuwapa.

‪“Naamini wananisikia, hivyo wamuachie na kama kuna taarifa zozote wanazoona zina makosa waniite mwenyewe kwa taratibu za serikali mimi nitawapa hizo taarifa,” amesema Zitto

Amesema kuna watu wamefikia kusema rasilimali fedha zake zote zinapita kwa Raphael ambapo amesema hahusiki na chochote ni vyema wakamuita mwenyewe kama hilo ndiyo dhumuni lao.

Akielezea namna alivyokutana na Raphael, Zitto amesema ni raia wa Kenya ambaye tangu mwaka 2002 alikuja nchini na alipata marafiki wengi wa Tanzania na hata kufunga ndoa na Mtanzania.

“‪Baada ya kuamua kuingia kwenye biashara aliendelea kuwa mtu wangu wa karibu na mpaka anatekwa tumekuwa bado ni watu wa karibu hakuwa anajihusisha na siasa kwa namna yoyote,” amesema Zitto.

Hata hivyo, Zitto amesema anawasihi watekaji hao wamuache Raphael mahali kisha wao watakwenda kumchukua.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles