30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

ZIMBABWE IMEJIBU, ACHA MAISHA YAENDELEE

NA MWANDISHI WETU

TUKIO la kutekwa kwa wasanii wa Bongo Fleva, Ibrahim Musa ‘Roma MkatoLiki’, Mon wa Centrozone, Bin Laden na kijana wa kazi wakiwa studio za Tongwe, jijini Dar es Salaam, hakuna aliyekuwa na jibu la nani hasa ni mhusika wa tukio hilo.

Ni jambo ambalo kwenye mazingira halisi ni ngumu kutokea, hasa katika nchi yenye amani kama Tanzania, wengi tuliingiwa na hofu, wasanii walikusanyika makundi kwa makundi kujadili hatma ya wenzao, viongozi walitoa matamko ya kuhakikisha Roma na wenzake wanapatikana wakiwa salama.

Hatimaye walipatikana wakiwa hai, ila wakawa kwenye maumivu makali ya mwili yaliyotokana na kupigwa na wateka nyara hao. Walitoa taarifa kituo cha Polisi Oysterbay, wakaenda hospitali kucheki afya zao na siku iliyofuata wakakutana na waandishi wa habari kuzunguza yaliyowakuta.

Licha ya Roma kuzungumza kile kilichotokea, mashabiki na jamii kwa ujumla bado ilibaki na maswali mengi yenye utata, ambayo Roma alishindwa kuyajibu alipoulizwa na wanahabari, hata yale ambayo hakuulizwa kutokana na unyeti wa sakata lenyewe.

Wengi wetu tulitarajia ipo siku ukweli halisi utajulikana, tuliamini kama siyo Roma, basi wale wenzake wanaweza kuja kuzungumza ukweli kwa njia yoyote ile, maana maswali yalikuwa mengi kuliko majibu yaliyotolewa siku ile wasanii hao walipokutana na waandishi wa habari.

Roma anafahamika kwa muziki wake wa harakati, hivyo matarajio ya kuumwaga ukweli yalikuwa makubwa zaidi. Tulitegemea ataongea ukweli kupitia wimbo, hatukujua ni wimbo gani na atautoa lini, maana tayari wengine walianza kusema baada ya kutekwa Roma, atabadilisha uelekeo wa muziki wake.

Lakini haikuwa hivyo, Roma ni msanii ambaye hana jukwaa la kuzungumza yaliyojaa kifuani mwake, hivyo kwa sanaa yake ameamua kutumia wino kuandika wimbo wa Zimbabwe, ambao una mafumbo mengi, hivyo unahitaji tafakuri ili upate majibu ya yale maswali ambayo wengi walikuwa nayo.

Wimbo umetengenezwa pale pale studio za Tongwe na prodyuza mdogo ambaye naye alitekwa, Binladen, na video kuongozwa na Nickclas huko Dodoma, maeneo ya Msembeta, njia ya kwenda Singida.

Baada ya hayo yote, acha maisha yaendelee, na hivi sasa ikiwa ni siku chache baada ya kuachia Zimbabwe, Roma na Stamina wametoka na wimbo wao mpya unaoitwa Hivi ama Vile, uliofungua ukurasa mpya wa maisha.

NUKUU

‘Tupo karne 21, itakuja karne ya 22, hizi zote tunaziita nyakati au vipindi vya watu kuishi na kuondoka, acha kujiona kwamba zama hizi zote zinakuhusu,”

Mrisho Mpoto.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles