27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

ZIJUE SABABU ZA MTOTO KUKOSA USINGIZI

Na Aziza Masoud

ILI mtoto aweze kukua vizuri anapaswa kuwekewa utaratibu mzuri wa kulala mchana na usiku.

Mtoto asiyepata usingizi vizuri anakuwa hatarini kupata madhara mbalimbali ikiwemo kudumaa akili.

Ripoti kamili ya matokeo ya utafiti wa jarida la afya la Sleep yaliyotolewa Aprili 2007 yanaeleza kuwa wataalamu wa masuala ya afya ya usingizi wanashauri watu wazima kupata wastani wa angalau saa saba mpaka nane za kulala kila usiku ili kuwa na afya bora.

Kwa kuzingatia hilo mzazi anapaswa kuwa na utaratibu na ratiba madhubuti kuhakikisha mtoto anapata muda mrefu wa kupumzika kwa nyakati za mchana na usiku.

Katika ratiba za mtoto kuna haja ya kuweka utaratibu ambao utamjenga kujua muda wake maalumu wa kulala kwa nyakati za mchana na usiku.

Katika ratiba hiyo pia inapaswa kwenda sambamba na kuwekea mazingira ya mtoto kulala,wapo watoto wanaoshindwa kupata usingizi mchana kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kucheza, mtoto wa aina hiyo anaweza kudhibitiwa kwa kumbadilishia ratiba zake za mchana.

Pia kuna kundi la watoto ambao wanashindwa kulala nyakati za usiku jambo ambalo si la kawaida kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo za kimazingira.

Inaelezwa kuwa kitaalamu kuwa mazingira ya malazi kwa mtoto yanaweza kuchangia kukosa usingizi nyakati za usiku.

Aidha matatizo ya kutopata usingizi kwa mtoto yanaelezwa kuwa ni sababu za kibailojia huku  maambukizi katika masikio ambayo yanamfanya mtoto kuwa na maumivu nayo yanatajwa  kuhusika.

Chanzo kingine ni wazazi wenyewe kutopata usingizi hasa wale ambao ni mara ya kwanza kupata mtoto.

Mara nyingi wazazi wa aina hiyo hutumia muda mwingi kukaa na watoto nyakati za usiku jambo linalochangia kumfanya  mtoto kubadilisha ratiba ya kulala.

Jambo jingine linaloweza kumfanya mtoto ashindwe kulala ni mazingira ya chumba chake cha kulala, chumba kinaweza kuwa na hali ya baridi sana ama joto wakati wa usiku.

Mazingira mengine yanayochangia mtoto kutopata usingizi ni kumlaza kwenye chumba chenye giza nene, hali hiyo humsababishia mtoto kuwa na woga.

Chumba cha mtoto kukaa katika mazingira ya kelele kama vile karibu na mashine ama kiwanda chenye kelele.

Ni muhimu mzazi kuhakikisha mambo muhimu yanayomweka mtoto katika hali nzuri ya ukuaji ikiwamo kupata muda wa kulala yanazingatiwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles