24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

ZIFF wafungua pazia waanza kupokea filamu za 2016

???????????????????????????????NA FESTO POLEA

KAMATI ya maandalizi ya Tamasha la Kimataifa la Filamu Zanzibar (ZIFF), imetangaza kuanza kupokea filamu za wasanii mbalimbali kote duniani ili zishindanishwe na kupitishwa kwa ajili ya kuonyeshwa katika tamasha hilo kwa mwakani.

Mkurugenzi wa Tamasha hilo, Prof Martin Mhando, alisema licha ya uwepo wa hofu ya kutokuwepo kwa matamasha makubwa yanayofanyika visiwani Zanzibar, tamasha hilo la 18 lenye kauli mbiu ya ‘Ndiyo hii Safari Yetu’ litafanyika kama kawaida kuanzia Julai 9 hadi 17 mwaka 2016 katika viwanja vya Ngome Kongwe visiwani humo.

“Naamini kukosekana kwa tamasha la Sauti za Busara lililotakiwa kufanyika Februari mwakani wengi wanaweza kuingiwa na hofu kwamba tamasha la Ziff nalo linaweza kutofanyika, hivyo waondoe hofu lakini pia tunaiomba Serikali ya Zanzibar na Tanzania kwa ujumla kusaidia matamasha haya yafanyike kama yanavyopangwa kwa kuwa yanaiingizia pato kubwa Serikali na kutangaza utalii wake kutokana na kuwa na wageni wengi kutoka sehemu mbalimbali duniani,’’ alisema Prof. Mhando.

Aliongeza kwamba, kila mwaka tamasha la ZIFF hupokea zaidi ya filamu 60 kutoka Afrika Mashariki ya Kati, Ulaya, Latin America, Marekani na Asia.

Filamu zinazopokelewa ni makala, filamu ndefu, filamu fupi, filamu za katuni, nchi za Jahazi, Filamu za Afrika Mashariki na video za muziki kutoka kwa wasanii wa Afrika Mashariki.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles