24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

ZIDANE KUPEWA MKATABA WA MAISHA

MADRID, HISPANIA


BAADA ya klabu ya Real Madrid kufanikiwa kutwaa Ligi ya Mabingwa Ulaya juzi dhidi ya Juventus kwa kuifunga mabao 4-1, Rais wa timu hiyo, Florentino Perez, amefunguka na kusema kocha wao Zinedine Zidane atapewa mkataba hadi mwisho wa maisha yake.

Kocha huyo kwa kipindi cha siku 512 alizokaa ndani ya kikosi hicho ikiwa ni mwaka mmoja na miezi mitano, amekuwa na mafanikio makubwa na kuufurahisha uongozi pamoja na mashabiki wa timu hiyo.

Tangu ajiunge ndani ya Santiago Bernabeu, Januari 9, 2016 hadi sasa ameweza kutwaa mataji mawili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Ligi Kuu nchini Hispania msimu huu, Uefa Super Cup mara moja na Kombe la Dunia la klabu.

Kutwaa Ligi ya Mabingwa Ulaya mara mbili ni historia mpya kwa Madrid pamoja na kocha huyo ikiwa mara ya mwisho kutokea ni 1958.

“Naweza kusema Zidane ataendelea kuwa ndani ya Real Madrid hadi mwisho wa maisha yake, kila shabiki wa Madrid leo hii anajivunia kuwa na mtu wa aina hiyo.

“Alianza kuwa hapa kama mchezaji tangu mwaka 2001, aliweza kuwa na mchango mkubwa wa mafanikio hadi anastaafu soka, leo hii amekuwa kocha wa timu hiyo na anaendelea kufanya makubwa zaidi.

“Ninaamini kwa sasa yeye ni kocha bora duniani, amekuwa na sisi kama kocha kwa miezi 17 na tayari ametuaminisha kuwa kila kitu kinawezekana kwa kutwaa mataji makubwa,” alisema Perez.

Awali wakati anapewa timu hiyo na kutwaa ubingwa huo kwa mara ya kwanza, Perez alimwambia kwamba ahakikishe anatwaa Ligi Kuu nchini humo na kama atashindwa basi milango itakuwa wazi kuondoka.

Kwa upande wake, Zidane amedai hana uhakika kama ataendelea kuwa ndani ya kikosi hicho hadi mwisho wa maisha yake, lakini anashukuru kwa yale anayofanyiwa na uongozi wa klabu hiyo.

“Siwezi kusema kwamba nitakuwa hapa hadi mwisho wa maisha yangu, lakini nina furaha kubwa kutokana na sapoti ninayoipata. Nimecheza soka hapa kwa muda mrefu na ninajiona kuwa miongoni mwa bidhaa za timu hii, furaha yangu ni kuona nilikuwa sehemu ya timu na sasa nipo kama kocha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles