25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Zanzibar Heroes, Kili Stars kazini Chalenji

2-5NA ZAINAB IDDY

MICHUANO ya Chalenji inayoshirikisha nchi za Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (Cecafa), inatarajia kuanza leo nchini Ethiopia huku timu ya taifa ya Zanzibar ‘Zanzibar Heroes’ ikianza kibarua kwa kuvaana na Burundi huku wenzao wa Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’ wakicheza kesho kwa kucheza na Somalia.

Michuano hiyo inayoanza leo itamalizika Desemba 6 mwaka huu ambapo Zanzibar Heroes inayonolewa na Kocha mkuu, Hemed Morocco, akisaidiana na Malale Hamsini, ipo kundi B pamoja na Uganda na mabingwa watetezi, Kenya.

Kilimanjaro Stars inanolewa na Kocha mkuu, Abdallah Kibaden, akisaidiwa na Juma Mgunda, imepangwa kundi A ikiwa na Rwanda, Somalia na wenyeji Ethiopia.

Tayari Kibadeni amesisitiza kuweka rekodi kwa kutwaa taji hilo na pia kutoa mfungaji bora katika kikosi hicho.

“Tunakwenda Ethiopia kwa lengo moja la kupambana na sio kushiriki, nina imani uwezo tunao licha ya kukosa muda wa kufanya maandalizi ya kutosha, ila kuwepo pamoja kwa wachezaji wengi waliokuwa Taifa Stars kutasaidia kufanya vizuri,” alisema.

Kikosi cha Kilimanjaro Stars tayari kimewasili Addis Ababa jana alfajiri kikiwa na wachezaji 18 pamoja na viongozi tayari kwa mashindano hayo.

Wachezaji waliosafiri na timu hiyo ni makipa, Ally Mustafa na Aishi Manula, walinzi, Shomari Kapombe, Kessy Radmahani, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’, Hassan Isihaka, Salim Mbonde na Kelvin Yondani.

Wengine ni viungo, Himid Mao, Salum Abubakar, Jonas Mkude, Salum Telela na Said Ndemla, huku safu ya ushambuliaji ikiongozwa na Malimi Busungu, Elias Maguli, Simon Msuva, Deus Kaseke na nahodha, John Bocco.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles