24.5 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Zaidi ya watu 4000 nchini hukatwa miguu kwa kisukari

MWANDISHI WETU

Kampuni ya Mawasiliano ya Abel & Fernandes imeungana na Kampuni ya  Afya ya AAR na wadau wengine kwa lengo la kushirikiana na Serikali katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa kisukari ambao umeelezwa kusababisha zaidi ya watu 4,000 kukatwa miguu kwa mwaka.

Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni hiyo jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Abel & Fernandes, Fatma Fernandes alisema kampeni hiyo dhidi ya kisukari imelenga kuboresha huduma za afya na maisha ya watu wanaoishi na ugonjwa huo.

Alisema kampeni hiyo iliyopewa kaulimbiu ya ‘Tenda Leo, Mabadiliko ya Kesho …tuungane kutokomeza kisukari’ imelenga kuwaunganisha wadau mbalimbali kuboresha huduma za kinga, tiba ili kudhibiti ugonjwa wa kisukari.

Alisema watatoa huduma kwa mamia ya jamii iliyokumbwa na kisukari, kutoa taarifa muhimu kuhusu kisukari na kupaza sauti kwa wale waliokosa haki zao dhidi ya ugonjwa wa sukari.

“Ugonjwa wa kisukari nchini unakua, kwa sababu hadi sasa watu zaidi ya milioni 4.2 wamebainika kuwa na ugonjwa huo. Abel & Fernandes tunaelewa tatizo hili, ndio maana tumeamua kuungana kuelimisha watu juu ya ugonjwa huo ili waweze kupata matibabu sahihi na kujua namna ya kujitunza,” alisema.

Alisema ili kufikia malengo  hayo ya uhamasishaji, Abel & Fernandes inakusudia kufanya kazi na madaktari na wataalam ili kuhakikisha kuwa huduma sahihi zinatolewa katika hospitali mbalimbali kwa walioathirika na ugonjwa huo.

Aidha, naye Dk. Akil Msei kutoka AAR alisema kwa mujibu wa ripoti za Shirika la Afya Duniani (WHO) takwimu zinaonyesha kila sekunde 10 mtu mmoja mwenye kisukari hufariki duniani na zaidi ya watu 40,000 wenye kisukari Tanzania hukatwa miguu.

Alisema pia zaidi ya watu milioni 422 wana kisukari duniani  hivyo kupelekea ugonjwa huu kushika nafasi ya 5 kama kisababishi cha vifo duniani.

 “Ugonjwa wa kisukari ni ugonjwa sugu na unaathiri watu wengi. Kuna aina mbili za ugonjwa wa kisukari; Aina ya 1 na Aina ya 2. Aina ya 2 inazuilika na hii ndio tunajaribu kushughulikia ili tuweze kuzuia kuongezeka kwa visa kama hivyo. “

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles