27.1 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Zaidi ya watoto 150,000 kupatiwa chanjo tatu Bariadi

Derick Milton, Bariadi

Zaidi ya watoto 150,000 wenye umri wa kuanzia miezi tisa hadi miaka mitano katika Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, wanatarajiwa kupatiwa chanjo ya magonjwa ya Surua, Lubela na Polio.

Chanjo hizo zitaanza kutolewa Septemba 26 hadi 30, mwaka huu katika zahanati, vituo vya Afya na hospitali mbalimbali kwenye wilaya hiyo, ambapo wananchi wamehimizwa kujitokeza kwa wingi kwani chanjo hizo zinatolewa bure.

Mratibu wa Chanjo katika halmashuari ya Mji wa Bariadi Marko Igenge akizungumza katika kikao cha kamati ya Afya ya msingi Wilaya leo, amesema kuwa siku zote tano zitatumika kutoa chanjo hizo kwa walengwa.

Amesema kuwa katika chanzo ya surua na lubella watoto wote wenye umri wa kuanzia miezi tisa hadi miaka mitano ndiyo watapewa chanjo hizo, huku chanjo ya polio watoto watakaohusika ni wale wenye miezi 18 hadi 42.

“Chanjo hizi ni muhimu sana kwa watoto wanachi wajitokeza kwa wingi kuleta watoto wao, surua na lubella uambukizwa kwa njia ya hewa hivyo watoto wanakuwa kwenye hatari zaidi,” amesema Igenge.

Kaimu mganga mkuu wa halmashuari hiyo Dk. Said Mlowosha aliwaomba viongozi wa dini pamoja na kamati hiyo ya Afya kuhasisha jamii ili kuweza kuleta watoto wao waweze kupata chanjo ambazo ni kinga ya magonjwa hayo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles