Imechapishwa: Mon, Sep 4th, 2017

ZAIDI YA NYUMBA 150 KUBOMOLEWA TANGA

Na Amina Omari-Tanga

HALMASHAURI ya Jiji la Tanga inatarajia kubomoa nyumba zaidi ya 150 zilizojengwa na wananchi kwa kuvamia maeneo isivyo halali na kusababisha migogoro ya ardhi.

Azimio hilo lilitolewa na   Meya wa Jiji hilo, Suleiman Mustafa wakati wa kikao cha kawaida cha baraza la madiwani juzi.

Alisema   maamuzi ulifikiwa  baada ya wananchi kuvamia maeneo  holela na kuanza ujenzi bila ya kufuata taratibu za mipango miji, hususani katika eneo la uwanja wa ndege na Ram Singh.

“Hatutaweza kumuonea mtu katika hiyo bomoabomoa kwa sababu  tumejipanga kuhakikisha wavamizi wote wa maeneo   tunawaondoa ili kuondoa kero ya uvamizi wa maeneo,” alisema Meya Mustafa.

Mkurungenzi Mtendaji wa Jiji la Tanga, Daudi Mayeji alisema   wamejipanga kuwachukulia hatua watendaji wa mitaa na kata waliohusika   kuuza maeneo ya ardhi bila ya kufuata taratibu.

Alisema  uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa kuna baadhi ya watendaji wamehusika katika kuuza maeneo wakati sheria haiwaruhusu kufanya hivyo.

“Nikiri kuwa migogoro mingi ya maeneo ya ardhi imesababishwa na baadhi ya watendaji wa halmashauri wasio waaminifu.

“Lakini sasa tunaanza operesheni, tukibaini mtendaji kuhusika na kuuza maeneo tutamchukulia hatua za  nidhamu,” alisema mkurungenzi huyo.

Weka maoni yako

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>

YOUTUBE

ZAIDI YA NYUMBA 150 KUBOMOLEWA TANGA