30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Zahera aliamsha ‘dude’ Arusha

MOHAMED KASSARA -DAR ES SALAAM

KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amewata wachezaji wa timu hiyo kuongeza umakini katika kufuatilia mbinu anazowapa mazoezini, ili waweze kufanya vizuri katika mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Township Rollers.

Yanga ililazimishwa sare ya bao 1-1 Rollers ya Botswana nyumbani, katika mchezo wa kwanza wa hatua ya awali Ligi ya Mabingwa Afrika uliochezwa Jumamosi iliyopita Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mchezo wa marudiano utapigwa Agosti 24 jijini Gaborone, ambapo Yanga inahitaji ushindi au sare ya mabao kuanzia 2-2, ili kutinga raundi ya kwanza.

Katika kuhakikisha wanafanya vizuri kwenye mchezo huo, Yanga imeamua kuweka kambi jijini Arusha, kwa ajili ya kuzoea hali ya hewa ya baridi ambayo inafanana na ya jijini Gaborone wakati huu.

Ikiwa Kanda ya Kaskazini, Yanga imepanga kucheza michezo miwili ya kirafiki dhidi ya timu za Polisi Tanzania utakaochezwa kesho na AFC Leopard ya Kenya utakaochezwa Jumapili.

Kikosi hicho kilitua Arusha juzi na kuweka makazi Hoteli ya Panama Resort kabla ya jana asubuhi kuanza mazoezi kwenye Uwanja wa Moreni jijini humo, kwa ajili ya kujiandaa patashika ya ugenini.

Katika mazoezi hayo, Zahera alionekana kuwa mkali kwa wachezaji wake ambao hawafuati maelekezo yake katika kila zoezi alilolitoa, huku akiwataka kuongeza umakini zaidi.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Mratibu wa timu hiyo, Hafidh Saleh alisema wamepokelewa vizuri na mashabiki wao wa Arusha na tayari wameanza kujifua.

Alisema kocha wao huyo amewataka wachezaji wake kuongeza umakini katika mazoezi hayo ili kushika kwa haraka mbinu anazowapa kuelekea mchezo huo wa marudiano.

“Tunashukuru kwa mapokezi makubwa tuliyopata hapa Arusha, tumeona kiu ya mashabiki wetu ambao walikuwa hawajatuona kwa muda mrefu, kikosi kilifika jana (juzi) na bila kupoteza muda wachezaji walianza kufanya mazoezi.

Mazoezi hayo yaliendelea leo asubuhi (jana) na jioni, kila mchezaji anaoneka kuwa kwenye hali nzuri na kujiamini, lakini Zahera ameongeza msisitizo zaidi kwenye mazoezi akiwataka wachezaji kuacha utani wafuate maelekezo anayowapa,”alisema.

“Zahera amepanga kuhakikisha washambuliaji wake wanaelewana kabla ya mchezo huo, kwa hiyo amepanga kuhakikisha anatumia michezo hiyo miwili ya kirafiki kumaliza tatizo la ushambuliaji ili watakapokwenda ugenini wapate ushindi wa kishindo.”

Saleh alisema Zahera amefurahishwa na kurejea kwa Juma Abdul na Kelvin Yondani kwenye kikosi chake kwakua kumeongeza hamasa kuelekea mchezo wao na Township.

“Kutokana na uzoefu walionao wachezaji hao, ni wazi timu inakwenda kunufaika na kurejea kwao,Yondani ameongeza mzuka zaidi kwenye eneo la beki wa kati, Juma nae atakuwa msaada mkubwa kwenye beki ya kulia baada ya Paulo Godfrey ‘Boxer’ kuumia na kubakia Dar es Salaam,”alisema Saleh ambaye kabla kushika wadhifa huo alikuwa meneja wa kikosi hicho..

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles