27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

YAYA TOURE ATUMA UJUMBE FIFA

LONDON, England

KIUNGO wa kati wa Manchester City,  Yaya Toure, amesema kuwa, Kombe la Dunia la mwaka ujao linalotarajiwa kufanyika nchini Urusi litashindwa pakubwa iwapo litatawaliwa na ubaguzi wa rangi.

Toure, mwenye umri wa miaka 34, alikabiliwa na matamshi ya ubaguzi wa rangi wakati Manchester City ilipocheza dhidi ya CSKA Moscow katika mchezo wa Klabu Bingwa uliochezwa nchini Urusi mwaka 2013.

“Tunatakiwa kuona mabadiliko kwa sababu watu wamekuwa wakizungumza kuhusu jambo hilo la ubaguzi, lakini hakuna anayejali wala kujishughulisha nalo,” alisema Toure.

Kiungo huo anataka kulisaidia Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) na Serikali ya Urusi kukabiliana na tatizo hilo kabla ya michuano hiyo kuanza rasmi.

“Lazima tuone mabadiliko kwa sababu hawalizungumzii suala hili na kupewa utatuzi,” aliongeza Toure.

Mwezi uliopita, Liverpool ililalamika kwa Uefa kuhusu madai ya matamshi ya ubaguzi wa rangi yaliyomlenga winga Bobby Adekanye, wakati wa mechi ya Kombe la Uefa upande wa vijana katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Spartak Moscow.

“Kila mmoja wetu anaizungumzia Urusi, lakini natarajia mambo yatakuwa tofauti na tunavyofikiria kwa kila mtu kujaribu kufanya kila kitu kiende vizuri nchini Urusi,” alisema Toure.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles