23.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

YANGA YENYE SURA MPYA YAANZA KUSAKWA

 WINFRIDA MTOI – DAR ES SALAAM 

KLABU ya Yanga, imezindua rasmi mchakato wa kuelekea katika mfumo wa mabadiliko ya uendeshaji wa klabu hiyo. 

Mchakato huo utasimamiwa na kamati ndogo inayoongozwa na Mwanasheria, Alex Mgongolwa. 

Kampeni hiyo ilizinduliwa jana jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Yanga, Dk Mshindo Msolla, ikiwa ni rasmi kuanza kupokea maoni ya wanachama. 

Yanga imefikia hatua hiyo, baada ya kukamilisha makubaliano na wataalamu kutoka Ligi Kuu Hispania (La Liga), Hispania, kupitia andiko la awali la kamati ya ndogo ya mabadiliko. 

Akizungumzia uzinduzi huo, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Yanga, Hassan Bumbuli, alisema wanakwenda katika mfumo wa mabadiliko ilikuwa moja ahadi za viongozi wa klabu hiyo wakati wanagombea. 

Alisema mchakato huo utafadhiliwa na wadhamini wao, kampuni ya GSM na kauli mbiu yake ni ‘Twenzetu Kwenye Mabadiliko,” alisema Bumbuli. 

Alieleza kuwa uzinduzi huo ni mwanzo wa mambo mazuri yanayokuja katika klabu hiyo. 

Katika video ya Mwenyekiti wa Yanga, Dkt. Mshindo Msolla, iliyowekwa na katika mtandao wa klabu hiyo, alisikika akisema “Moja ya dhamila yangu wakati nagombea ni kubadilisha muundo wa uendeshaji wa klabu, nadhani ndoto hiyo inakwenda kukamilika. 

“Ombi la viongozi kwa wanachama na wapenzi wa Yanga, tuwe

 kitu kimoja, tuungane na uongozi na wadhamini ili tuweze kufanikisha hilo, Yanga moja katika Twenzetu Kwenye Mabadiliko,” alisema.

Alisema uzinduzi huo, ni mwanzo wa kuelekea katika mabadiliko ambao utakuwa muda rasmi wa mchakato wa kufika kule wanakotaka kwenda.

Kwa upande wake, Mkugenzi wa uwekezaji wa GSM, Hersi Said, alisema watajitoa kwa hali na mali kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa kama walivyoahidi kudhamini mchakato huo katika hatua ya awali.

Alisema kilichokuwa kinasubiriwa ni makubaliano ya kimkataba ya pande mbili, kati ya watu kutoka La Liga na Yanga, jambo ambalo limeshakamilika.

“Kama tulivyoahidi kusaidia katika mchakato huu wa mabadiliko, tutafanya hivyo kuhakikisha mabadiliko yanakwenda vizuri na kila Mwanayanga anapata nafasi ya kutoa maoni yake,”alisema. 

Alisema hatua, iliyofikiwa ni nzuri kutokana na vikao vilivyokuwa vinafanyika muda mefu, kuweka mipango sawa, anaamini kila kitu kitakwenda vizuri baada ya uzinduzi.

Katika udhamini huo wa mchakato wa mabadiliko, GSM waliahidi kutoa ofisi itakayotumiwa na wataalam hao kutoka Hispania, pindi wakatapowasili nchini.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles