26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Yanga wavamia anga anga za Alliance

*Watamba kuwatuliza wenyeji wao Alliance kama ilivyokuwa kwa Mbao FC

THERESIA GASPER-DAR ES SALAAM

KIKOSI cha Yanga kimewasili salama jana mkoani Mwanza, kikiwa tayari kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Alliance, utakaochezwa kesho Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Yanga ilisafiri kuifuata Alliance, ikiwa na kikosi cha wachezaji 20.


Vijana hao wa Jangwani watakutana na Alliance wakiwa na kumbukumbu ya kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mbao FC, katika mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa kwenye dimba hilo.

Lakini walijiongezea hali ya kujiamini, baada ya kufuzu robo fainali ya Kombe la Shirikisho (ASFC), baada ya kuindoa mashindanoni Namungo FC ikiichapa bao 1-0, mchezo uliochezwa Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Mratibu wa kikosi cha Yanga, Hafidh Salehe, alisema kikosi chao kimewasili salama jijini Mwanza tayari kwa mchezo wao wa kesho dhidi ya Alliance.

 “Tumefika salama Mwanza, wachezaji watapumzika kidogo lakini jioni watafanya mazoezi Uwanja wa Nyamagana, kocha wetu, Mwinyi Zahera, atatumia fursa hiyo kuyafanyia kazi baadhi ya mapungufu kabla ya kuwakabili Alliance,” alisema.

Alisema wachezaji wao wote waliosafiri na timu hiyo wapo timamu kimwili na kiakili kwa ajili ya kuhakikisha wanakipigania kikosi hicho na kushinda.

“Morali ya kikosi kwa ujumla iko juu, kila mchezaji anataka kutoa mchango ambao utaiwezesha timu kupata ushindi, pia hakuna majeruhi jambo ambalo linampa wigo mpana kocha wa kuamua aanze nani,” alisema Hafidh ambaye kabla ya kuteuliwa kushika wadhifa huo alikuwa meneja wa kikosi hicho.

Timu hizo zilipokutana katika mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Alliance.

Yanga pia inaongoza msimamo wa Ligi Kuu, ikiwa na pointi 61, baada ya kucheza michezo 25, ikishinda 19, sare nne na kupoteza miwili.

Alliance ambayo inashiriki ligi hiyo kwa mara ya kwanza baada ya kufuzu  msimu uliopita, ipo nafasi ya saba, ikiwa na pointi 36, baada ya kucheza michezo 28, ikishinda tisa, sare tisa na kuchapwa mara 10.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles