23.3 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Yanga waelekeza nguvu robo fainali ASFC

YNA WINFRIDA MTOI

KIKOSI cha Yanga kinatarajia kuanza mazoezi kesho, kujiandaa na mechi ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho (ASFC) dhidi ya Alliance FC, utakaopigwa Machi 30, mwaka huu Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Tayari kikosi cha Yanga kimerejea jijini Dar es Salaam, kikitokea mkoani Iringa ambako kilikwenda kuikabili Lipuli FC katika mchezo wake wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa Jumamosi iliyopita dimba la Samora na kufungwa bao 1-0.

Yanga ilifuzu robo fainali, baada ya kufanikiwa kuiondosha mashindanoni  Namungo FC, kwa kuifunga bao 1-0, mchezo uliochezwa Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa, mkoani Lindi.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Mratibu wa Yanga, Hafidh Saleh, alisema baada ya kutoka Iringa waliwapa wachezaji wao mapumziko ya siku mbili ambayo yatafikia tamati leo kabla ya kesho kuendelea na mazoezi Uwanja wa Chuo cha Polisi Kurasini, Dar es Salaam.

Saleh alisema kocha msaidizi wa kikosi hicho, Noel Mwandila, ataendelea na programu alizoachiwa na kocha mkuu wao, Mwinyi Zahera, ambaye ametimkia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ambako ana majukumu ya kuinoa timu ya Taifa ya nchi hiyo, akiwa na dhamana ya kocha msaidizi.

“Tuna siku nyingi za maandalizi ndiyo sababu tumeona tupumzike kwa siku hizi chache, wachezaji walioitwa timu ya Taifa tumewaruhusu, lakini waliobaki  tutaendelea na mazoezi Jumatano kwa ajili ya mechi ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Alliance FC.”

Alisema wanafanya maandalizi ya uhakika kwa lengo la kuhakikisha wanashinda mchezo wao dhidi ya Alliance, kwa kuwa lengo ni kusonga mbele na hatimaye kutwaa ubingwa.

“Kila mmoja anatambua umuhimu wa mchezo huo ili kutimiza malengo tuliyojiwekea, maandalizi yataendelea huku tukisubiri wachezaji waliopo katika kikosi cha timu ya taifa kabla ya kuelekea Mwanza,” alisema.

Alisema wana matumaini hadi kufikia siku ya mechi hiyo, kocha mkuu atakuwa tayari amerejea nchini, kwa kuwa ratiba za mechi za timu za Taifa zitakamilika  kabla ya michezo Kombe la Shirikisho kuanza.

Wachezaji wa Yanga waliopo katika majukumu ya timu ya Taifa ni Faisal Salum Abdallah (Fei Toto), Gadiel Michael na Kelvin Yondani, ambao waliingia kambini jana kujiandaa na mechi ya kuzufu Fainali za Kombe la Mataifa Afrika (Afcon) dhidi ya Uganda itakayochezwa Machi 24, 2019 kwenye Uwanja wa Taifa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles