31.7 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Yanga, Simba,TFF zajadili kauli ya Kabwili

Winfrida Mtoi – Dar es Salaam

KLABU  ya Yanga, Simba na Shirikisho la Soka Tanzania(TFF)zimezungumzia kauli ya kipa Ramadhan Kabwili kuwa aliwahi kuahidiwa gari aina ya Toyota IST endapo angeukosa mchezo wa Watani hao wa Jadi.

Kabwili alitoa kauli wakati wa mahojiano yake na kituo kimoja cha redio jijini Dar es Salaam juzi.

Katika mahojiano hayo, kipa huyo wa Yanga  alidai aliwahi kufuatwa na viongozi wa Simba na kumtaka kufanya vitendo vitakavyosababisha alimwe kadi ya njano na kukosa mchezo dhidi yao wa msimu uliopita kwa ahadi ya kupatiwa IST.

Kabwili alidai alitakiwa kufanya hivyo kwakua tayari alikuwa na kadi mbili za njano hivyo kama angepata nyingine na kufanya idadi kuwa tatu angekosa mchezo dhidi ya Yanga, kwakua kanuni za mashindano za TFF haziruhusu.

Kutokana na kauli hiyo, uongozi wa Simba umeibuka na kupinga vikali ukidai kauli ya kipa huyo inaashiria kuwapo kwa upangaji wa matokeo kitu ambacho hakikubaliki.

Taarifa ya Simba iliyolewa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, Senzo Mbata, inasema tuhuma hizo zina  madhara makubwa katika uadilifu wa klabu hiyo na viongozi wake.

“Klabu ya Simba inafurahishwa na hatua za haraka zilizochukuliwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), juu ya kauli hiyo, tunaamini hatua stahiki zitachukuliwa,” ilisema taarifa hiyo.

Ofisa Habari wa TFF, Cliford Ndimbo, alisema taasisi hiyo imeandika barua Kamati ya Maadili kufuatilia jambo hilo.

Alisema pia watavijulisha vyombo vingine vya usalama ili kusaidia uchunguzi na baada ya kubaini ukweli  hatua stahiki zitachukuliwa.

Naye Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Yanga, Hassan Bumbuli, alisema mchezaji wao huyo alitakiwa kushauriana na viongozi wake kabla ya kutoa kauli hiyo kwenye vyombo vya habari.

Bumbuli alisema licha ya kuwa wachezaji wao hawaruhusiwi kuzungumza na vyombo vya habari bila ruhusa, watampa ushirikiano Kabwili kwa kuwa tayari limeshatokea.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles