25.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

YANGA MMECHELEWA

NA ZAINAB IDDY


JUMATATU iliyopita uongozi wa timu ya Yanga ulizindua utaratibu wa wanachama wake kuweza kuichangia fedha klabu yao, zitakazotumika katika masuala ya uendeshaji wa timu hizo.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwassa alisema utaratibu huo unameanza rasmi na mwanachama naweza kuichangia timu kuanzia kiasi cha 1000 katika mitandao yote ya simu za mkononi,  huku kampuni nya Selcom, ikibeba jukumu la ukusanyaji wa michango hiyo.

Ni jambo zuri na la kuigwa walilolifanya Yanga, ingawa wanaonekana kuchelewa mno kuanza kulingana na ukubwa wa timu yenyewe.

Yanga imeanzishwa zaidi ya miaka 80 iliyopita, lakini hadi sasa haina chanzo maalumu cha mapato kiasi cha kusababisha kuwepo na migomo isiyo na ulazima kutokana na wachezaji kudai fedha zao.

Kiroho safi inahakika kuwa iwapo Yanga wangeanza mpango huu mapema, timu hiyo kubwa na maarufu barani Afrika isingeweza kufikia hatua ya kudharaulika kama ilivyo hivi sasa.

Mfano mdogo tu Yanga inadaiwa kuwa na mashabiki si chini milioni sita, iwapo kama kila mmoja angekuwa anaichangia  kiasi cha Shilingi 100 kila siku, ndani ya siku 30 timu hiyo ingeweza kukusanya kiasi cha Sh milioni 18 je ndani ya miezi 12 ni kiasi gani wangepata.?

Huo ni mfano mdogo sana, ambao kwa maisha ya Watanzania hususani wapenda soka hawashindwi kuchangia timu wanayoipenda kiasi cha 500 hadi 1000 kwa siku, ambayo  kwenye uendeshaji wa timu si ndogo.

Ni wazi kama watachanga 500 kila mmoja, basi kwa mwezi zitakusanywa  Sh milioni 90,wakati kwa 1000 ingepatikana Sh milioni 18  je kwa miezi 12 kiasi gani kingepatikana?

Hata kama zisingetosha, lakini zingeweza kusaidia kupunguza masuala ya mishahara ya wachezaji, usafiri au kuanzisha mradi mkubwa utakaoingiza kipato cha kumaliza matatizo ya Yanga kwa ujumla.

Kuanza mchakato huo sasa ni wazi Yanga  mmechelewa sana, kwani ninahakika suala hili lingefanyika katika kuanzia miaka 50 iliyopita,Yanga ombaomba ya leo isingekuwepo.

Ni jambo la aibu kuona timu kubwa na kongwe wachezaji wake wakiweka migomo kwa kutolipwa mishahara, wakati kuna watu wanaoweza kutatua matatizo hayo.

Pongezi kwa Yanga kukumbuka hili, japo mmechelewa, lakini uchangishaji huu usiwe njia ya kufungua malumbano baina ya viongozi na wanachama, baada ya fedha zinazokusanywa kushindwa kufanya kazi iliyokusudiwa.

Wakati Kiroho safi ikiipongeza Yanga, ni wakati wa timu nyingine nazo kufuata nyayo za Wanajangwani hao kwani wanachama na mashabiki ni njia bora ya kujiongezea kipato, iwapo kama timu inaweza kujiendesha kwa uwazi.

Kwa wanachokifanya Yanga sitarajii kuona timu za Simba, Mbeya City na Mtibwa Sugar zikilia ukata wakati ipo fursa ya kuiigizia kipato.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles