24.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

YANGA KUIBOMOA SINGIDA UNITED

NA SAADA SALIM- ZANZIBAR

YANGA imeanza kufungua jicho lake katika usajili mkubwa, ambapo tayari jina la beki wa kushoto wa Singida United, Shafiq Batambuze, limetua mikononi mwa kocha mkuu wa timu hiyo, George Lwandamina.

Batambuze amekuwa chachu ya mafanikio ya Singida United katika Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu tangu alipotua katika kikosi cha timu hiyo wakati wa dirisha kubwa la usajili.

Taarifa za uhakika zilizoifikia MTANZANIA jana kutoka kwa kigogo mmoja wa Yanga, zinasema kiwango cha maana kinachoonyeshwa na beki huyo katika michuano ya Mapinduzi na Ligi Kuu Tanzania Bara, kimewashawishi kuliwasilisha jina lake katika benchi la ufundi ili kuangalia uwezekano wa kumsajili.

Alisema wanaamini beki huyo ataziba vema pengo la Haji Mwinyi ambaye anatakiwa na AFC Leopards ya Kenya.

“Ni beki mzuri, nimefanikiwa kumwona katika mechi nyingi anazocheza, yupo vizuri, pia ni muhimu kwetu kuja kuchukua nafasi ya Haji aliyepata ofa Kenya,” alisema.

Kigogo huyo alisema AFC Leopards bado wanamuwinda beki wao huyo, hatua inayowashawishi kutafuta mbadala wake mapema ambaye ni Mutambuze.

Beki huyo alipoulizwa kuhusiana na uwezekano wa kuhamia Yanga, alisema haoni tatizo kama wataafikiana kwa kuwa soka ni kazi yake.

“Kwa kuwa mkataba wangu unaniruhusu kuzungumza na timu nyingine waje tuzungumze, lakini kwa sasa sitaongea chochote,” alisema Mutambuze.

Kuhusu dau analohitaji alisema hawezi kuliweka wazi hadi Yanga watakapozungumza na kukubaliana.

MTANZANIA halikuishia hapo, lilimtafuta Mwenyekiti wa Leopards, Daniel Mule, ambaye alisema mpango wa kumsajili Haji upo pale pale.

“Tunasubiri dirisha kubwa Juni tuanze mchakato wa kuingia mkataba na beki huyo wa Yanga,” alisema Mule.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles