27.5 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Yanga, KMC nani ameiva?

Na WINFRIDA MTOI, DAR ES SALAAM

KIKOSI cha Yanga kinatarajia kushuka dimbani leo katika mchezo wa kirafiki dhidi ya KMC, utakaopigwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Wanajangwani hao tangu wameanza mazoezi ya kujiandaa na mwendelezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu ni zaidi ya wiki moja sasa, wakijifua Uwanja wa Chuo cha Sheria jijini hapa.

Kabla ya kuivaa KMC, Yanga iliumana na Transit Camp na kuibuka na ushindi wa mabao 3-1, mchezo uliorindima katika uwanja huo.

Mara ya mwisho ya Yanga ilikutana na KMC katika mchezo wa Ligi Kuu uliochezwa Machi 12, dimba Uhuru.

Katika mchezo hio, KMC iliibuka mbabe kwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0.

KMC kama  ilivyo kwa Yanga, inajiweka sawa kwa mwendelezo wa Ligi Kuu utakaoanza Juni 13.

Yanga itaendeleza kampeni zake za ligi hiyo kwa kuumana na Mwadui FC, Uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga, wakati KMC itapepetana na Ruvu Shooting, mchezo utakaopigwa Juni 20 mwaka huu Uwanja wa Uhuru.

Akizungumzia mchezo huo, Kocha Msaidizi wa Yanga, Charles Mkwasa anayekinoa kikosi hicho kwa sasa, alisema wameamua kucheza na KMC kwa sababu ni timu yenye kiwango kinachoweza kuwapima nyota wake.

Mkwasa alisema, mchezo huo ni muhimu katika kuangalia ni wapi wamefikia tangu walipoanza mazoezi na hawatacheza mechi nyingine baada ya leo, badala yake watajiandaa na safari ya Shinyanga.

“Huu mchezo utakuwa wa kujipima nguvu , tumefanya nini katika mazoezi, tulianza kucheza na Transit Camp, tumeshinda 3-1, lakini bado nahitaji mchezo mkubwa zaidi hivyo KMC ni sahihi kwetu.

“Ukitaja kati ya timu zenye ushindani katika Ligi Kuu, KMC ni mojawapo, ninaamini utakuwa ni mchezo mzuri na mgumu, pia mashabiki wa Yanga watapata nafasi ya kuona kikosi chao,” alisema Mkwasa.

Kuhusu maendeleo ya kikosi hicho, alisema kwa sasa wameingia katika program ya kuchezea mpira na ndiyo sababu wakahitaji michezo ya kirafiki.

“Nahitaji kuwafanya wachezaji wawe fiti na stamina ya hali ya juu kutokana na mechi zinazotukabili ni ngumu, unajua kukaa bila kucheza au kufanya mazoezi muda mrefu imeturudisha nyuma,” alisema Mkwasa.

Alisema wachezaji wake wamerejea mazoezini kila mmoja akiwa tofauti, wapo waliongezeka uzito, kutokana na kushindwa kuzingatia  program walizopewa.

Mkwasa aliwataka miongoni mwa wachezaji wake walioongezeka uzito kuwa kwa mujibu wa ripoti ya daktari wa klabu hiyo kuwa ni  David Molinga aliyeongezeka kilogram 12, Yikpe Gislain kilogram 10, Patrick Sibomana kilogram saba na Said Juma Makapu kilogram sita.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles