30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Yanga, Azam shughuli pevu

Theresia Gasper -Dar es salaam

YANGA itashuka dimbani leo kuumana na Azam FC,  katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, utakaochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Yanga itashuka dimbani ikiwa na jeraha la kuchapwa mabao 3-0 na Kagera Sugar, katika mchezo wake uliopita uliochezwa dimba la Uhuru, Dar es Salaam.

Azam kwa upande wao itakuwa vizuri kisaikolojia baada ya kuitungua Lipuli mabao 2-0, katika mchezo wake uliopita  uliochezwa dimba la Taifa.

Wanajangwani hao wanashika nafasi ya nane katika msimamo wa Ligi Ku, wakijikusanyia pointi 25 katika michezo 13 waliyoshuka dimbani, wakishinda saba, sare nne na kupoteza miwili.

Azam yenye inakamata nafasi ya tatu, ikijikusanyia pointi 29, katika michezoi 14 iliyoshuka dimbani, ikishinda tisa, sare mbili na kupoteza mara tatu.

Timu hizo zilipokutana msimu uliopita, Yanga ilishinda bao 1-0 mzunguko wa kwanza kabla ya Azam kushinda mabao 2-0 mzunguko wa pili, mechi zote zikipigwa Uwanja wa Taifa.

Yanga itashuka dimbani ikiwa na hasira ya kutaka ushindi kutokana na matokeo mabaya iliyoyapata katika mchezo uliopita.

Hata hivyo itaendelea kumkosa mshambuliaji wake Tariq Seif ambaye anauguza majeraha pamoja na kiungo Mohammed Issa ‘Banka’ anayetumikia adhabu ya kadi nyekundu.

Azam itashuka dimbani ikihitaji kuendeleza ushindi lakini itawakosa mabeki wake Yakubu Mohammed anayetumikia adhabu ya kadi tatu za njano na Agrey Morris ambaye hivi karibuni alipata msiba wa mkewe.

Pia haitakuwa na kiungo Mudathir Yahya yupo Falme za Kiarabu(UAE) akifanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa.

Akizungumzia mchezo huo, Kocha Msaidizi wa Azam, Idd Nasoro ‘Cheche’, alisema kila mchezo wanaingia uwanjani na mfumo mpya, hilo litajitokeza pia watakavyoikabili Yanga, lengo likiwa kuvuna pointi tatu.

“Tumejiandaa kiushindani kwani nafahamu mchezo utakuwa mgumu na ukizingatia wapinzani wetu mchezo uliopita hawakupata matokeo mazuri hivyo umakini unahitajika zaidi,” alisema.

Kocha Mkuu wa Yanga, Luc Eymael amesema wana kila sababu ya kupambana kwa nguvu na kushinda mchezo huo ili kurejesha morali ya kikosi chake baada ya kupoteza mchezo uliopita.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles