31.7 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

WOSIC yatoa elimu ya kupinga ukatili wa kijinsia kwa wafanyabiashara

Lulu Ringo, Dar es Salaam     

Shirika la Kupinga, Kukataa na Kutokomeza Ukatili wa Kijinsia kwa Wanawake (WOSIC), limefanya mkutano na wafanyabiashara wa soko la Magomeni Usalama, Dar es salaam kwa ajili ya kutoa elimu kwa wafanyakazi wa soko hilo jinsi ya kutokomeza unyanyasaji huo kwa wafanyabiashara wa wanawake wa soko hilo.

Akizungumza na wafanyabiashara hao leo Ijumaa Novemba 30, mtoa mada wa kutoka katika shirika hilo, Shabani Ruhimbiye, amesema kumekuwa na unyanyasaji mkubwa kwa wanawake wanaofanya biashara katika masoko na wengi wao kufanyiwa ukatili wa kingono, kisaikolojia na kiuchumi hali inayosababisha wanawake hao kushindwa kufanya biashara zao kwa uhuru.

“Wafanyabiashara wa kike wamekuwa wakinyanyasika wanapokuwa katika majukumu yao ya kibiashara, wengine wananyimwa haki zao kama fedha za malipo ya manunuzi ya bidhaa zao wakishurutishwa kufanya vitendo vya ngono kwa ajili ya kupata haki wanayostahili, wengine wamekuwa wakiitwa majina ya ajabu kutokana na maumbile yao.

“Inabidi ifike wakati wanawake waheshimike na kuonekama wana thamani katika jamii, pia wapewe fursa nyingi kama wanaume, mfano fursa ya kuwa viongozi wa soko hili kama ilivyo kwa wanaume ambapo kwa sasa viongozi ni wanaume kwa asilimia 95,” amesema Ruhimbiye.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Mradi huo, Mossy Ismail, ameeleza kuwa Januari mwaka huu WOSIC ilipata ufadhili wa Shirika la Mfuko wa Maendeleo Afrika (AWDF) na kuanzisha  mradi wa haki ya mwanamke sokoni, ikiwa soko la Magomeni Usalama ndilo soko pekee lililopata elimu hiyo hadi sasa.

“Hadi sasa tumetoa elimu hii katika Soko la Magomeni tu, tulianza Januari mwaka huu na tulianza kwa kutoa elimu kwa wanawake na uongozi wa soko na leo ndiyo tumefanya mkutano wa nje kwa ajili ya kutoa elimu kwa wafanyabiasha wote,” amesema Mossy.

Mkutano huo uliosindikizwa na maigizo mbalimbali ya kupinga unyanyasaji huo, kutoka kwa wanafunzi wa Chuo cha Sanaa Bagamoyo (Kaole), ulionekana kuwa na mwitikio mkubwa hasa kwa upande wa wanaume waliotoa ahadi ya kuacha na kutokomeza kabisa  unyanyasaji kwa wanawake hao.

 

 

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles