23.3 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

World Vision yashauri wanawake kujifungulia zahanati

Eliya Mbonea, Arusha

Wananchi wa Kijiji cha Losingori wilayani Monduli mkoani Arusha wametakiwa kuanza kujifungulia kwenye Kituo cha Afya ya Uzazi lililojengwa Zahanati ya Losimingori badala ya kujifungulia majumbani.

Ushauri huo umetolewa na Shirika la World Vision Tanzania liliojenga jengo hilo lililogharimu Sh milioni 51.3 ambapo lilichangia Sh milioni 38.7 huku jamii ikichangia Sh milioni 10 na Shirika la HIMS Sh milioni moja.

Akizungumza wakati wa kukabidhi jengo hilo kwa Halmashauri ya wilaya ya Monduli, Mtaalamu wa miradi ya kiuchumi Kanda ya Babati World Vision, Rahel Pazzia aliitaka jamii hiyo ya kifugaji kuanza kutumia jengo hilo.

“World Vision tunataka hadi ifikapo mwaka 2030 tuwe tumewafikia watu wanaishi mazigira hatarishi, niwaombe mama zangu na akina baba mila potofu za kujifungulia nyumbani tuziache,” amesema Pazzia

Kwa upande wake Mwakilishi wa Mganga wa wilaya ya Monduli, Zaituni Kivuyo alisema kwa wilaya hiyo kuanzia Januari hadi Oktoba mwaka huu walijifungua akina mama 5,275 sawa na asilimia 80.

Naye Mkuu wa wilaya Iddi Kimanta alisema kukamilika kwa jengo hio kutawasiti akina mama waliokuwa wanashindwa kwenda kujifungua Zahanati ya Losimingori.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles