Imechapishwa: Tue, Mar 13th, 2018

WOLPER KUWEKEZA KIMATAIFA

NA JESSCA NANGAWE


STAA wa Bongo Movie na mjasiriamali maarufu, Jackline Wolper, amesema pamoja na mafanikio anayoyapata kwa sasa kupitia duka lake la mavazi, anachofikiria kwa sasa ni kuongeza matawi zaidi ndani na nje ya nchi.

Wolper ambaye mbali ya uigizaji anamiliki duka la mavazi maarufu kama Wolperstlish, amesema anashukuru Mungu kuona kazi yake hiyo ikizidi kufanya vizuri na kumpatia wateja lukuki kutokana na ubora wa kazi hali iliyomfanya kutamani kuongeza matawi zaidi nje ya Tanzania.

“Najivunia kazi ninayofanya, imekuwa ikinizalishia wateja kila kukicha, imefikia kipindi sasa natamani kufanya kazi Kenya, Uganda na kwingine ili niweze kujitangaza na hata kuitangaza nchi yangu kupitia mavazi ninayoyaandaa,” alisema Wolper.

Wolper alisema kwa sasa anafikiri zaidi kuanzisha maduka mengine nje ya Mkoa wa Dar es Salaam baada ya kupata wateja mbalimbali wa mikoani huku akisisitiza ni biashara ambayo hakutegemea ingemwongezea thamani kwa haraka kama ilivyokuwa.

Weka maoni yako

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>

YOUTUBE

WOLPER KUWEKEZA KIMATAIFA