26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

WMA kuvuna milioni 600 za uhifadhi

Mwandishi Wetu, Meatu

Hifadhi ya Jamii ya Wanyamapori (WMA) ya Makao, wilayani Meatu mkoani Simiyu kwa miaka mitano ijayo inatarajia kuanza kupokea Sh milioni 600.

Licha ya kupokea fedha hizo, WMA hiyo ilipokea msaada wa gari aina ya Toyota Land Cruiser baada ya kusaini mkataba wa miaka mitano wa utalii na uwindaji na Kampuni ya Mwiba Holdings.

Akizungumza wakati wa kusaini mkataba huo, Meneja wa Mwiba Holdings moja ya kampuni za Friedkin Conservation Fund, Mark Ghaui, amesema wanatarajia kwa miaka mitano ijayo kuongeza watalii.

“Ni imani yetu gari hilo lenye thamani ya Sh milioni 40, litasaidia katika doria za ulinzi wa wanyamapori na mazingira,” amesema.

Naye Katibu wa Makao WMA, Robert Simon alitangaza kuanza kwa operesheni ya kuondoa wavamizi maeneo ya hifadhi.

“Tumetoa mwezi mmoja kwa kaya zaidi ya 60 zilizovamia maeneo ya hifadhi ziondoke haraka, mkataba tuliosaini umeboresha mapato kutoka milioni 400 hadi 600 na fedha za kila kijiji zitakuwa wastani wa Sh milioni 27 kutoka Sh milioni 25,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles