WIZKID KUFUNGUA DUKA MAREKANI

0
525

 

NEW YORK, MAREKANI


STAA wa muziki nchini Nigeria, Ayodeji Balogun maarufu kwa jina la Wizkid, ametangaza kufungua duka la nguo jijini New York, nchini Marekani.

Msanii huyo ambaye amefanya kazi na wasanii mbalimbali nchini Marekani, kama vile Drake, Chris Brown, Nicki Minaj na wengine, amedai duka hilo litakuwa linaitwa ‘Star Boy clothing collection.’

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, msanii huyo aliposti baadhi ya picha za duka hilo na nguo zilizopo ndani huku akidai kuwa litafunguliwa muda mfupi kuanzia sasa.

Hata hivyo, amedai endapo atafanikiwa na duka hilo, basi atahakikisha anafanya hivyo kwenye nchi mbalimbali kwa ajili ya kuwafikia mashabiki wake.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here