23.8 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Wizara zakutana kujadili kamera kudhibiti uhalifu

Na MWANDISHI WETU-ZANZIBAR


WIZARA ya Mambo ya Ndani ya Nchi na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalumu za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,  zimekutana kujadili suala la kufunga kamera maalumu za kudhibiti na kuzuia uhalifu.

Akizungumza wakati wa kikao hicho, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni alisema Serikali inatambua umuhimu wa ulinzi na usalama kwa raia wake na iko katika mpango wa kufunga kamera hizo katika miji yote mikuu nchini.

Alisema lengo la kufunga kamera hizo ni kuiwezesha serikali kupambana na matukio ya uhalifu ya utekaji, makosa ya barabarani, uporaji wa fedha katika taasisi za fedha.

“Tumekuja kuchukua uzoefu kwa wenzetu wa Zanzibar ambao tayari wameshafunga kamera hizi katika maeneo mbalimbali na nimeona jinsi zinavyofanya kazi za kubaini wahalifu.

“Teknokolojia haiepukiki katika kudhibiti, Serikali tumejipanga na hivi karibuni tutaanza kufunga kamera za CCTV  katika miji mikuu na maeneo ya mikoa iliyoko mipakani   kudhibiti wahalifu kutoka nje ya Tanzania,” alisema Masauni

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalumu za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Radhiya Rashid Haroub alisema tayari washafunga kamera hizo ambazo zilizinduliwa Oktoba 3, mwaka huu.

Alisema uzinduzi wa kamera hizo ulifanywa na Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles