Imechapishwa: Mon, Jun 4th, 2018

WIZARA YA FEDHA YAOMBA TRILIONI 12

Elizabeth Hombo, Dodoma


Wizara ya Fedha na Mipango imeliomba Bunge liidhinishie makadirio ya mapato na matumizi ya Sh trilioni 12, ili iweze kutekeleza majukumu yake kwa mwaka wa fedha 2018/2019, kwa mafungu yote nane yaliyo chini ya wizara hiyo.

Maombi hayo yametolewa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizaya hiyo, Bungeni jijini Dodoma, leo.

Dk. Mpango amesema kati ya fedha hizo Sh trilioni 10 ni kwa ajili matumizi ya kawaida na Sh trilioni moja kwa ajili ya maendeleo.

Weka maoni yako

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>

YOUTUBE

WIZARA YA FEDHA YAOMBA TRILIONI 12