33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

WIZARA YA ARDHI YAPIMA VIWANJA MILIONI MOJA KWA MIAKA 50

Justo Lyamuya
Justo Lyamuya

JOHANES RESPICHIUS-DAR ES SALAAM

TANGU nchi ipate uhuru mwaka 1961, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeweza kupima viwanja milioni 1.36,  mashamba 24,579  na vijiji 10,667.

Hayo yalibainishwa na Mkurugenzi wa Idara ya Upimaji na Ramani, Justo Lyamuya alipozungumza  na waandishi wa habari  Dar es Salaam jana.

Alisema mwaka wa fedha 2016/17 lipo lengo la kupima na kutoa hati 400,000 na  kampuni zinazopima ardhi zinatakiwa kushirikiana na Serikali kuhakikisha lengo hilo linafanikiwa.

“Kwenye robo ya kwanza ya mwaka wa kuanzia Julai hadi Septemba 2016 umefanyika upimaji wa viwanja 32,303 na mashamba 76 ingawa upimaji mashamba umekuwa ukipungua huku viwanja vikiongezeka kutokana na maeneo mengi kugeuka kuwa ya mpango.

“Pia kuhusu upimaji wa ardhi ya maji, kwa kipindi cha miaka mitatu, Tanzania kwa kushirikiana na Jeshi la Maji la India imeweza kupima Bandari ya Dar es Salaam, Zanzibar na mkoani Pemba na kwa mwaka huu umefanyika upimaji wa bandari ya Tanga,” alisema Lyamuya.

Alisema tayari imekwisha kuandaliwa  mikataba ya makubaliano na kuridhiwa kupima mipaka ya kimataifa yote ya bandarini na majirani.

Kuhusu  maziwa makubaliano ya kweka mpaka ndani ya ziwa Tanganyika kati ya Tanzania, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Zambia na Burundi yameshafanywa na utekelezaji wake utaanza fedha zikipatikana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles