WIZ KHALIFA AMWANIKA MPENZI MPYA

0
174

NEW YORK, MAREKANI


HATIMAYE mkali wa muziki wa hip hop nchini Marekani, Wiz Khalifa, amemwanika mpenzi wake mpya baada ya kuachana na mama mtoto wake, Amber Rose mwaka 2014.

Wiz Khalifa na Amber Rose walifanikiwa kufunga ndoa 2013, lakini walikuja kuachana mwaka mmoja baadaye huku wakifanikiwa kupata mtoto mmoja. Tangu kuachana huko Wiz Khalifa hakuwahi kumwanika mpenzi mpya, lakini mwishoni mwa wiki iliyopita aliamua kumtambulisha mwanamitindo Winnie Harlow kuwa ni mpenzi wake.

Msanii huyo mbali na kuachana na mama wa mtoto wake, lakini walionekana kuwa karibu katika kumlea mtoto wao na kuwafanya mashabiki wadhani kuwa wapo kwenye mipango ya kutaka kurudiana.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa rapa huyo, aliposti picha akiwa na Winnie na chini yake kuandika maneno ambayo yalionesha wazi wawili hao wapo kwenye uhusiano.

“Wiz na Winnie  ni wapenzi,” aliandika msanii huyo akiambatanisha na picha mbili za kopa zikionesha alama ya upendo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here