WIZ KHALIFA AMPANDISHA MWANAYE ‘SCHOOL BUS’

0
503NEW YORK, MAREKANI

RAPA Wizkhalifa, ametikisa mitandao ya kijamii mwishoni mwa wiki iliopita baada ya kuposti picha akiwa na mtoto wake mwenye umri wa miaka mitano Sebastian, wanasubiri basi la shule.

Mashabiki walimshambulia msanii huyo kutokana na utajiri alionao na kumuacha mtoto wake akienda shule siku ya kwanza kwa kutumia usafiri wa basi la shule badala ya kumpeleka na gari yake au kumkodia tax.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, msanii huyo aliposti picha hiyo na kuandika, “Siku ya kwanza ya Kindergarten. Tukisubiri basi la shule!!.,”

Hata hivyo msanii huyo aliwajibu wale wote ambao walimshambulia kwenye ukurasa huo kwa kusema “Kuwa tajiri hakuweza kukufanya kwenda sawa na wakipendacho watoto. Watu wengi wamekuwa wakiniuliza kwa nini nimemuacha mtoto wangu akipanda basi la shule wakati mimi ni tajiri.

“Nimefanya hivyo kwa makusudi, ninataka mwanangu apate uzoefu wa kuwa na rafiki zake, hivyo tunatakiwa kuwaacha watoto wafanye kile wakitakacho,” aliandika Wizkhalifa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here