WILL, JADA WAMSAIDIA TYRESE

0
45

NEW YORK, MAREKANI


MKALI wa muziki na filamu nchini Marekani, Tyrese Gibson, amethibitisha kusaidiwa kiasi cha dola milioni 5 (zaidi ya bilioni 11) kutoka kwa Will Smith na mke wake Jada Pinkett.

Fedha hizo wamezitoa kwa ajili ya kumsaidia msanii huyo ambaye kamaliza kesi yake anayotuhumiwa kumpiga mtoto wake mwenye umri wa miaka 10.

Mama wa mtoto huyo, Norma Mitchell, alimfikisha baba mtoto wake katika kitengo cha huduma za watoto na familia jijini Los Angeles na kumshtaki, hata hivyo Tyrese aliweka wazi kuwa hajawahi kufanya jambo lolote baya kwa mwanaye kama inavyodaiwa.

“Namshukuru sana Will na mke wake Jada kwa kunipa kiasi cha dola milioni 5, ninaamini kweli wao wapo na mimi katika hali yoyote, wapo wengi ambao wanaonesha sapoti yao juu ya jambo hili lakini kwa Will na Jada kweli nyinyi ni wajomba zangu, asanteni sana,” aliandika Tyrese.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here