31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Wilaya ya Kipolisi Mbagala yapewa magari matatu

BUNGE limeelezwa kuwa  Jeshi  la Polisi limetoa magari matatu kwa wilaya ya kipolisi ya Mbagala na kufanya  wilaya hiyo kuwa na magari tisa.

Kauli hiyo ilitolewa jana bungeni na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Hamad Masauni alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Mbagala, Issa Mangungu(CCM).

Katika swali lake,Mangungu alidai kwamba Serikali ilianzisha Kanda Maalum ya Kipolisi,Dar es salaam na kufanya Wilaya ya Temeke kuwa Mkoa wa Kipolisi,tangu Temeke  iwe Mkoa wa Kipolisi hivyo kumekuwa na ongezeko kubwa la uhalifu.

Mbunge huyo alihoji Serikali ina mpango gani wa kujenga kituo cha Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Mbagala.

Mangungu alihoji,Serikali ina mpango gani wa kuanzisha vituo vya Polisi na kuviongezea askari vitendea kazi na kujenga nyumba za askari katika maeneo ya Jimbo la Mbagala.

Akijibu,Masauni alisema Wilaya ya Mbagala ni Wilaya mpya ya kipolisi iliyopo katika Mkoa wa Kipolisio wa Temeke .

Alisema kama ilivyo kwa Wilaya nyingine katika Kanda maalum ya Dar-es-Salaam Wilaya ya Mbagara inastahili kujengewa chenye hadhi ya Wialaya.

Alisema kwa sasa wananchi wa Mbagala wanahudumiwa katika kituo cha Polisi cha Mbagala Kizuiani  ambacho miundombinu yake haitoshelezi.

Aidha hali halisi ya kibajeti itakaporuhusu Serikali   itaweka mpango wa kuwajengea wananchi kituo kipya vya Polisi, nyumba za makazi na askari na ofisi ya Mkuu wa Polisi wa Mbagala.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles