26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

WILAYA 55 ZADAIWA KUKABILIWA  NA UPUNGUFU WA CHAKULA

Na Sam Bahari-Shinyanga



WAKATI wilaya 55 zikidaiwa kukabiliwa na upungufu wa chakula, Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula  (NFRA) ana  akiba ya mahindi tani 86,443.


Akitoa taarifa kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa NFRA,  Deusdedit Mpazi alisema kiasi hicho cha mahindi kimehifadhiwa katika maghala yaliopo katika kanda kuu saba nchini.


Mpazi alizitaja kanda hizo kuwa ni   Arusha, Dodoma, Kipawa, Makambako, Shinyanga, Songea na Sumbawanga ambako kuna maghala 33.


Alisema maghala hayo 33 yana uwezo wa kuhifadhi nafaka tani 246,000 na yanahudumia mikoa 26   nchini.
Hhata hivyo alisema NFRA ina mpango wa kuongeza uwezo wa kuhifadhi tani 246,000 hadi kufikia tani 1,000,000 ifikapo mwaka 2024.
  Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi,  William  ole Nasha, alisema utekelezaji wa  mpango wa upanuzi wa mradi huo utaendeshwa kwa awamu mbili.


Alisema awamu ya kwanza Serikali imepanga kuongeza uwezo wa uhifadhi wa nafaka kutoka tani 246,000 hadi tani 500,000 na awamu ya pili ni kuongeza uwezo hadi kufikia tani 1,000,000 ifikapo mwaka 2024.


Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji,  Dk. Mary Nagu,  alisema NFRA ni lazima iondoe  urasimu   katika kuwahudumia wananchi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles