Widodo aelekea kushinda urais Indonesia

0
430

JAKARTA, INDONESIA
RAIS wa sasa wa Indonesia Joko Widodo anaelekea kutetea kiti chake katika uchaguzi wa rais dhidi ya mpinzani wake mkuu, jeenerali wa zamani Prabowo Subianto.
Hiyo ni kwa mujibu wa matokeo yasiyo rasmi baada ya upigaji kura kumalizika katika maeneo yote ya nchi hiyo ya visiwa 17,000 juzi.
Matokeo rasmi yatatangazwa mwezi ujao, lakini mlolongo wa matokeo kutoka mashirika ya kitafiti nchini hapa unaonesha Widodo anaongoza kwa asilimia 11.
Matokeo ya mashirika hayo yamethibitishwa kuwa ya kuaminika katika kutoa ishara ya mshindi katika chaguzi zilizopita, lakini Widodo amejizuia kujitangaza mshindi, akiwataka wafuasi wake kuwa watulivu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here