23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

WHO KUWANOA WASIMAMIA KANUNI ZA AFYA AFRIKA

Veronica Romwald, Dar es Salaam

Shirika la Afya Duniani, Kanda ya Afrika (WHO – Afrika), liwamekutanisha wataalamu wasimamizi wa Kanuni za Afya za Kimataifa (IHR) kutoka nchi 14 za Bara la Afrika.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo Aprili 24, Ofisa wa Idara ya Udhibiti na Ufuatiliaji wa Magonjwa wa WHO – Afrika, Grace Saguti amesema lengo la mkutano huo ni kuwajengea uwezo wataalamu hao katika kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa kanuni hiyo katika nchi zao pamoja na utoaji taarifa kwa wakati juu ya magonjwa hayo.

“Nchi zinajitahidi lakini tunahitaji kujengewa uwezo zaidi, ushirikiano upo katika kudhibiti magonjwa haya ingawa kuna changamoto kwamba unaweza kukutana maabara ya uchunguzi wa magonjwa ya binadamu upo juu kuliko uwezo wa maabara za uchunguzi wa magonjwa ya wanyama,” amesema.

Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi wa Kitengo cha Udhibiti na Ufuatiliaji wa Magonjwa wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Janeth Mgamba amesema miaka ya hivi karibuni Bara la Afrika limekuwa likikabiliwa na magonjwa ya mlipeleke katika nchi mbalimbali.

“Kutokana na hali hiyo tumeshuhudia baadhi ya nchi zikiweka zuio kwa mfano la muingiliano wa watu na hata usafirishaji wa bidhaa za vyakula ndiyo maana tunahitaji kujadiliana kuangalia namna tutakavyoweza kukabili magonjwa haya bila kuathiri masuala ya kibiashara katika nchi zetu,” amesema.

Wataalamu hao wanatoka nchini Tanzania, Kenya, Uganda, Eswatini, Afrika Kusini, Msumbiji, Nigeria na nyinginezo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles