25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

WENYEVITI WAWILI MBARONI KWA TUHUMA ZA MAUAJI

o-black-man-handcuffs-facebook

Na RENATHA KIPAKA – BUKOBA 

MWENYEKITI wa Serikali ya Kijiji cha Nyabihanga na Mwenyekiti wa Kitongoji cha Bihanga, wilayani Ngara, Mkoa wa Kagera, wanashikiliwa na Jeshi la Polisi, mkoani Kagera, kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya watu wawili wakazi wa wilayani humo.

Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Kagera, Agustino Ollomi, aliwambia waandishi wa habari juzi, kuwa watuhumiwa hao walikamatwa juzi baada ya mauaji hayo kutokea.

Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Nyabihanga, Eradi Batakanwa na Mwenyekiti wa Kitongoji cha Bihanga, Wilson Cosmas.

“Watuhumiwa walikamatwa juzi kutokana na tuhuma zinazowakabili za mauaji ya watu wawili ambao ni Mwalimu Audax Elias (34) na Sadoki Erenesti (15), wote wakazi wa Wilaya ya Ngara.

“Mnamo Desemba 17 mwaka huu, Audax Elias na Sadoki Ernesti, walifika katika Kijiji cha Nyabihanga, Kata ya Bukiliro, wilayani Ngara kwa lengo la kununua mbuzi na kuku wa biashara.

“Baada ya kufika kijijini hapo, wananchi walianza kuwashambulia wakidhani ni wezi wa kuku na mbuzi.

“Mwili wa Sadoki umepatikana jana baada ya ushirikianao wa wenyeviti hao na lakini mwili wa Audax unaendelea kutafutwa,” alisema Kamanda Ollomi.

Kamanda Ollomi aliwaomba wananchi kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi ili waliohusika kwenye tukio hilo, waweze kukamatwa kwani kuna wengine bado wanaendelea kutafutwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles