24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Wenger kukamilisha kikosi chake saa 48

Arsene Wenger
Arsene Wenger

LONDON, ENGLAND

KOCHA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger, amethibitisha kuwa anataka kukamilisha kikosi chake kwa kusajili wachezaji wawili kabla ya kufungwa kwa usajili keshokutwa.

Kikosi hicho hadi sasa kimecheza michezo mitatu ya ligi kuu na kutoka sare mmoja, akipoteza mmoja na kufungwa mmoja, matokeo hayo yamemfanya awe katika wakati mgumu kutokana na mashabiki kuanza kuizomea klabu hiyo.

Baadhi ya viongozi walimtaka kocha huyo kufanya usajili kwa ajili ya kukiweka kikosi hicho sawa katika msimu huu wa ligi kuu.

Nyota wa zamani wa timu hiyo, Patrick Vieira, ambaye kwa sasa ni kocha wa klabu ya New York City FC ya nchini Marekani, wiki iliyopita alisema Arsenal kwa sasa ina wachezaji ambao hawana uwezo wa kutwaa ubingwa tofauti na miaka iliyopita, hivyo Wenger anatakiwa kufanya usajili kwa ajili ya kuendana na ushindani uliopo.

Kutokana na maneno ya mashabiki na baadhi ya viongozi, kocha huyo ameweka wazi kuwa anataka kusajili wachezaji wawili wiki hii, baada ya kutenga kitita cha pauni milioni 50.

Beki wa klabu ya Valencia, Shkodran Mustafi, tayari amewasili jijini London kwa ajili ya vipimo na kumalizana na klabu hiyo kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili.

Nyota huyo wa timu ya taifa ya Ujerumani, atajiunga na klabu hiyo kwa kitita cha pauni milioni 35, huku kiasi kingine cha pauni milioni 15 kwa ajili ya kumsajili nyota wa klabu ya Deportivo de La Coruna ya nchini Hispania, Lucas Perez.

Hadi sasa Arsenal imetumia kiasi cha pauni milioni 90 kutokana na usajili uliofanywa kwa Granit Xhaka, Rob Holding na Taksuma Asano.

“Ninaamini kila kitu kitakuwa sawa muda mfupi kuanzia sasa, tayari wamefanyiwa vipimo, kilichobaki ni makubaliano ya mikataba.

“Ninaamini wiki hii kila kitu tutakiweka wazi kuhusiana na hatima ya wachezaji hao wawili, hivyo mashabiki wakae tayari kwa hilo,” alisema Wenger.

Siku zote Wenger amekuwa kocha wa mwisho katika kukamilisha kikosi chake wakati wa usajili, hivyo mashabiki wa timu hiyo wamezoea hali hiyo kila mwaka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles