26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

WENGER AMFANANISHA SANCHEZ NA MESSI

LONDON, England

KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger, ameelezea umuhimu wa mchezaji wake, Alexis Sanchez, kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Chile, kwamba ni kama ilivyokuwa kwa Lionel Messi, Zinedine Zidane na David Beckham, kwa timu zao.

Wenger alitoa kauli hiyo muda mfupi baada ya Chile kushindwa kufuzu michuano ya Kombe la Dunia, inayotarajiwa kufanyika mwakani nchini Urusi.

Chile ya Sanchez imeshindwa kufuzu michuano hiyo, baada ya kupokea kipigo cha 3-0 dhidi ya Brazil katika mechi ya mwisho iliyochezwa Jumanne iliyopita.

Wenger, ambaye timu yake itarejea Ligi Kuu kwa safari ya kwenda Watford leo,  alisema Sanchez ni miongoni mwa kundi la wachezaji ambao timu zao za taifa zimekuwa zikiwategemea, sawa na Zidane ilivyokuwa kwa Ufaransa, Beckham kwa Uingereza na Messi kwa Argentina.

“Naweza kusema katika kila kizazi kuna mchezaji anayebeba presha ya matarajio ya taifa lake,” Mfaransa huyo alisema.

“Kwa Ufaransa alikuwa Zidane. Uingereza alikuwa Beckham. Tulikuwa na wachezaji wengine kwenye timu, lakini alikuwa Beckham. Kwa nini siyo Steven Gerrard? Sijui. Lakini alikuwa Beckham.

“Kwa Chile ni Sanchez. Kwa Argentina ni Messi. Inaonekana katika kila timu ya taifa yupo mmoja anayebeba presha na kulinda timu yote kwa ujumla.

“Ni mtu anayependa majukumu. Wanapenda kuwa mstari wa mbele. Lakini kwa ujumla hili lina maana gani? Inamaanisha ni lazima wakubaliane na kushindwa pia.”

Sanchez (28), anahusishwa na tetesi za kuondoka Arsenal kwa muda mrefu, wakati nyota huyo akiwa kwenye mwaka wa mwisho kwenye mkataba wake na klabu hiyo.

“Yuko sawa katika kipindi kigumu. Chile wameshinda Copa America mara mbili na sasa wameshindwa kwenda Kombe la Dunia,” alisema Wenger.

“Sanchez atakuwa na umri wa miaka 29 mwisho wa mwaka huu, kwa hiyo Kombe lingine la Dunia atakuwa na miaka 33. Anatarajia kwenda. Kwa yakini ni jambo ambalo limemuumiza.

“Lakini naamini kucheza katika kiwango chake cha juu ni sehemu pia ya kukubali changamoto.”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles