Wema awashauri wasanii wenzake kutambua thamani zao

0
1327

Elizabeth Joachim ,Dar es Salaam

Muigizaji Wema Sepetu amewashauri wasanii wenzie kutengeneza malengo yao katika uigizaji ili waweze kujitangaza zaidi na kujulikana katika masoko ndani na nje ya nchi.

Akizungumza katika kongamano la waigizaji lililoandaliwa na Bodi ya Filamu wakishirikiana na Chama cha Waigizaji Taifa lililofanyika leo Aprili 15 Jijini Dar es Salaam , Wema amesema muda sasa umefika wa wasanii kujitengenezea thamani katika uigizaji.

“Wasanii tunatakiwa tuamke na tujue jinsi ya kujitengenezea uthamani wetu wa baadae kesho ukizeeka ukijiangalia bado unajiona unathamani katika jamii na thamani haiji yenyewe inakuja jinsi unavyojiweka na kukujitengeneza.

“Mwaka 2006 mimi Wema nilishinda taji la Miss Tanzania lakini nilianza kujulikana rasmi baada ya kujikita kwenye masuala ya uigizaji japo kuna mambo niliyafanya hapo katikati lakini thamani yangu inatambulika”,amesema Wema.

Aidha ameishukuru Bodi ya Filamu kwa kuandaa kongamano hilo na kuwakutanisha na wasanii ambao hawakuwa wamekutana muda mrefu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here